Itakuwaje na Tanzania wakipiga marufuku hili? - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Itakuwaje na Tanzania wakipiga marufuku hili?


Image copyrightReuters
Image captionGari la Volkswagen
Taifa la Uswizi limepiga marufuku kuuzwa kwa magari aina ya Volkswagen ambayo yana mitambo ya iliyotengenezwa kudanganya majaribio ya gesi chafu.
Idara inayosimamia usafiri wa barabarani nchini humo inasema kuwa hadi magari 180,000 yataathiriwa.
Hilo ndilo pigo la hivi punde kwa kampuni hiyo ya Ujerumani tangu ikiri kuwa magari milioni 11 yanayotumia mafuta ya diesel kote duniani yamewekwa mitambo inayuweza kudanganya kuhusu gesi chafu.
Mauzo ya hisa za kampuni ya Volkswagen yameshuka katika kipindi cha wiki moja tangu kufichuliwa kwa sakata hiyo.
Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Volkswagen amesema kuwa uchunguzi ulio wa kina na wazi utafanyika.chanzo bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages