Mpira umekwisha.
ChelseaFC 2-0 Arsenal
Kufuatia ushindi huu Chelsea sasa wamepanda hadi nafasi ya 10 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.
Arsenal wamesalia katika nafasi ya nne japo sasa wamo katika hatari ya kushuka iwapo wataendelea kupata matokeo kama haya.
4:36 ChelseaFC 2-0 Arsenal
GOOOOOOOOOOAL
@ChelseaFC 2-0 @Arsenal Eden Hazard 90''
Hazard anaupiga lakini wapi unakuwa mwingi na kutoka nje na kuwa ni Kona
Kona kuelekea lango la Arsenal
Fabregas ndiye anayeupiga
Freekick kuelekea lango la Arsenal nje tu ya eneo la lango
Kocha Jose Mourinho amesalia na dakika 10 tu kusajili ushindi wake wa pili katika ligi kuu ya Uingereza
Wapinzani wake Arsenal wamesalia 9 uwanjani.
Diego Costa anaondoka uwanjani anapumzika
Japo hakufunga bao, ndiye aliyechangia pakubwa kwa idadi ya wachezaji Arsenal kupungua uwanjani
4:24 ChelseaFC 1-0 Arsenal
Refarii Mike Dean anatoa kadi ya pili nyekundu dhidi ya mchezaji wa Arsenal Carzola
Arsenal wamesalia wachezaji 9 uwanjani.
Hazard anakosa
Hazarddddddddd !
Lo !
4:07 ChelseaFC 1-0 Arsenal
Kurt Zouma anaifungia Chelsea bao muhimu dhidi ya Arsenal kunako dakika ya 52 ya mechi hii
GOOOOOOOOAL
3:57 ChelseaFC 1-0 Arsenal
3:50 ChelseaFC 0-0 Arsenal
Kipindi cha pili kimeanza
Chelsea wakiwa na nguvu ya mtu mmoja zaidi wanawashambulia wapiga bunduki mapema
3:35 ChelseaFC 0-0 Arsenal
ChelseaFC 53% - 47% Arsenal
Kipindi cha kwanza kimekamilika bila ya bao lolote.
Arsenal hata hivyo watalazimika kubadili mipango kwani watakosa huduma za Gabriel katika kipindi cha pili.
3:35 ChelseaFC 0-0 Arsenal
Hii ni mara ya pili katika juma moja ambapo Arsenal wanajipata bila mchezaji mmoja uwanjani
Gabriel wa Arsenal anaoneshwa kadi Nyekundu.
Refaree Mike Dean anamuonesha kadi nyekundu kwa kuzozana na Mshambulizi wa Chelsea Diego Costa
3:29 ChelseaFC 0-0 Arsenal
Arsenal wanapoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la kwanza
Sasa Chelsea wanashambulia
3:19 ChelseaFC 0-0 Arsenal
Diego Costaaaaaa
Costa anapoteza nafasi nyengine ya wazi
Kwa hakika Chelsea inafanya mashambulizi kwenye lango la Arsenal
3:11 ChelseaFC 0-0 Arsenal
Diego Costa anashambulia lango la Arsenal
Diego Costaaaaaa
Tutumie ujumbe wako kupitia mtandao wa twitter
Tafuta BBCSwahili
kama msomaji wetu huyo Anjesco
Wapi,,,,,
Kipa nambari moja Peter Cech anaupakata mkwaju wa Costa
3:05 ChelseaFC 0-0 Arsenal
Nipe nikupe kati ya hazard na Costa nusura izae matunda
Lakini wapi
3:02@ChelseaFC 0-0 @Arsenal
2:57 '' @ChelseaFC 0-0 @Arsenal
Hatimaye Wenger alikubali salamu za mwenyeji wake Mourinho
Arsenal wanafanya mashambulizi ya mapema kuelekea lango la Wenyeji wao
2:53 ''Chelsea 0-0 Arsenal
Arsenal wanapata Kona ya kwanza
Konaaaa kuelekea upande wa Chelsea
2:45 Mpira umeanza !
Chelsea 0-0 Arsenal
Branislav Ivanovic anaiongoza Chelsea kuingia uwanjani Stamford Bridge.
John Terry leo hayuko
Leo anapasha benchi moto
Je hii ni dalili kuwa uhusiano wake na kocha Mourinho umezorota?
Kikosi cha Arsenal
33 Cech 24 BellerÃn 05 Gabriel 06 Koscielny 18 Monreal 34 Coquelin 19 Cazorla 16 Ramsey 11 Özil 17 Sánchez 14 Walcott
Wachezaji wa Akiba
02 Debuchy 03 Gibbs 08 Arteta 12 Giroud 13 Ospina 15 Oxlade-Chamberlain 21 Chambers
Kikosi cha Chelsea
01 Begovic 02 Ivanovic 24 Cahill 05 Zouma 28 Azpilicueta 04 FÃ bregas 21 Matic 17 Pedro 08 Oscar 10 Hazard 19 Diego Costa
Wachezaji wa Akiba
07 Ramires 09 Falcao 12 Mikel 18 Remy 26 Terry 27 Blackman 36 Loftus-Cheek
Kocha mbishi Jose Mourinho amemuonya mwenzake wa Arsenal, kuwa timu yake imerejesha makali yake na kuwa mechi ya leo huko darajani ama ukipenda Stamford Bridge itakuwa kiziba mkonga tu ya uamko mpya.
Hayo yanajiri magwiji hao wawili wakitokea kwenye kidumbwedumbwe cha kombe la mabingwa barani ulaya ambapo 'the Blues' walipata ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv.
Arsenal kwa upande wao walipigwa mabao mawili kwa moja mikononi mwa Dinamo Zagreb.
Licha ya usemi huo, Chelsea itakosa huduma za mshambulizi wake wa kati kati Willian kutokana na jeraha alilopata katika mechi hiyo ya katikati ya wiki.
hamstring .
Radamel Falcao, Oscar na Pedro huenda wakacheza ama wasicheze.
kwa upande mwengine,kipa nambari moja Petr Cech, atarejea katika uwanja anaoufahamu vyema tu wa Stamford Bridge baada ya kushuhudia kichapo dhidi ya Zagreb kutoka mbali.
Haijabainika iwapo Per Mertesacker atarejea baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.
Kufikia sasa Arsenal, wanashikilia nafasi ya 4 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza wakiwa wamecheza mechi 5 wakajishindia alama 10.
Chelsea kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 17 wakiwa wamecheza mechi 5 na kujizolea alama 4 pekee.
Chelsea wameshinda mechi moja pekee kufikia sasa.
Je mechi hii itakuwa na tofauti kwao ?
Ungana name katika matangazo ya moja kwa moja kati ya Chelsea na Arsenal.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)