Licha ya mtaa wa Mbweni JKT, jijini Dar es Salaam kujengwa majumba ya kifahari na kupatikana pia nyumba za viongozi mbalimbali wa serikali, miundo mbinu yake, hususan daraja linalojengwa katika eneo hilo ili kuwafanya wananchi wapite kwa urahisi kusua sua. Kwa miaka kadhaa sasa ujenzi wa daraja hilo umesimama.
Pichani ni gari la mwananchi na mkazi wa eneo hilo akipta kwenye maji ambayo mara kadhaa hujikuta wamesimama kwa saa kadhaa, hususan kama eneo hilo litajaa baada ya eneo hilo kujaa maji yanayotoka baharini.
Hali hiyo si tu inakwamisha maendeleo, pia ni hatari kwa usalama wa wananchi kwenye eneo hilo. Wananchi wengi wameonekana kuichoka hali hiyo na kuiomba serikali kulifanyia kazi daraja hilo ili kuwafanya wananchi waingie na kutoka bila usumbufu wowote kama unaotokea wakati huu.
Kambi ya JKT Mbweni ikiwa tulii. Ujenzi wa daraja hilo umekwama. Wananchi hawajui ujenzi huo umekwamia wapi. Baadhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu walimuomba Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda na Mkurugenzi wake kuangalia namna gani mradi huo umesimama kwa miaka mitatu sasa.
Linaloonekana nyuma ya kibao cha tangazo la Halmashauri ni daraja linalojengwa kwenye eneo la Mbweni JKT ambalo hata hivyo limesimama na kuleta adha kubwa kwa wakazi na wananchi wa eneo hilo kwa miaka mitatu sasa. Wananchi hao wameendelea kutaabika hasa sehemu hiyo inavyopokea maji mengi kutoka baharini kila wakati. Picha zote za Mpiga Picha Wetu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)