Mchezaji wa Taswa Fc, Julius Kihampa (kushoto) akikokota mpira wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha dhidi ya timu ya IMS Maji ya Chai, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Mchezaji
wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimdhibiti mchezaji wa timu ya Chuo cha waandishi wa Habari cha AJTC wakati wa mchezo wao. Katika mchezo huo Taswa
Queens, ilishinda mabao 37 - 3

Nahodha
wa timu ya Taswa Queens, Zuhura Abdulnoor, akipokea Kikombe cha ushindi kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya kutangazwa washindi wa
Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Baadhi
ya waandishi wa habari za Michezo kutoka Vyombo mbalimbali vya habari,
wanaounda timu ya Waandishi wa habari za Michezo Tanzania, Taswa Fc na Taswa
Queens, wakimsikiliza Afisa wa Hifadhi ya Michael Ngatolu, wakati walipotembelea kwenye hiyo,
walipokuwa katika ziara ya kuhitimisha Bonanza la 10 la Taswa Arusha
lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.

**********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Arusha
TIMU ya
Taswa Fc na ile ya Taswa Queens, zinazoundwa na wachezaji wa Habari za Michezo
kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, jana ilihitimisha ziara yake ya
siku mbili katika mikoa ya Arusha na Tanga.

Aidha timu
hiyo ilifanikiwa kumaliza ziara hiyo bila kufungwa huku Taswa Queens, wakiibuka
kidedea kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya Bonanza la Taswa Arusha
yanayofanyika kila mwaka, baada ya kuwagalagaza bila huruma timu ya Chuo cha
Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC kwa jumla ya mabao 37-3. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Wakati Taswa
Queens ikitwaa Kombe hilo, Taswa Fc, wao walimaliza bonanza hilo bila kufungwa
huku wakitoka sare katika michezo yake yote mitatu.

Katika
mchezo wa kwanza Taswa Fc ambayo ilidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro, ilitoka sare ya bila kufungana na timu ya ORS ya Manyara, kabla ya
kutoka sare ya bila kufungana tena na timu ya IMS Maji ya Chai, na baadaye
kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Kampuni ya Habari Maalum ya Arusha.

Baadaya
Bonanza hilo Taswa Fc, walielekea Tanga Segela na kucheza mchezo wake wa mwisho
na timu ya Kombaini ya Segera na Michungwani na kuibuka washindi kwa mabao 2-0
katika mchezo uliokuwa mkali na wa kuvutia kutokana na timu zote kucheza kwa
speed na kukamiana huku wachezaji wakionyesha uwezo wa hali ya juu.

wa Taswa Fc, Zahro Mlanzi, akimtoka mchezaji wa timu ya IMS Maji ya Chai,
wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa
wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Katika mchezo huo timu
hizo zilitoka sare ya 1-1.

Nahodha wa timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari AJTC, Jasmine Mumwi, akipokea zawadi ya fedha Sh. 150,000 ya mshindi wa pili katika Netiboli.
Mchezaji wa Taswa Fc, Martine Peter, akimtoka mchezaji wa timu ya IMS Maji ya Chai, wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Mkuu wa Mkoa Arusha akisoma hotuba yake ya kufunga Bonanza hilo.
Hussein Omari na Imman Makongoro wa Taswa Fc na Taswa Queens, wakifurahia baada ya kukamata Kuku katika mchezo wa kukimbiza kuku kwenye Bonanza la 10 la Taswa Arusha mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
Wachezaji wa Taswa Queens, wakipasha baada ya kumaliza mchezo wao na AJTC.
Mchezaji wa Taswa Queens, Sharifa, akimiliki mpira wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa akiba wa Taswa Queens.
Centre huyu ni noumer aisee...
Centre wa Taswa Queens, akiwahi kumiliki mpira...
Mchezaji wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimiliki mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC. Katika mchezo huo Taswa Queens, ilishinda mabao 37 - 3.
Zutta, wa Taswa Queens, akimiliki mpira
Mwenyekiti wa Taswa Majuto Omary, akipokea zawadi ya fedha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya timu yake kutangazwa kuwa timu yenye nidhamu katika mashindao ya Bonanza la 10 la Taswa Arusha, lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Nahodha wa timu ya Taswa Queens, Zuhura Abdulnoor, akipokea zawadi ya Sh. 150,000, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, baada ya kutangazwa washindi wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kikosi cha Taswa Queens...
Wachezaji wa Taswa Fc na Taswa Queens wakiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha Taswa Queens na kombe lao
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)