Pages

RAIS KIKWETE AZINDUZA KIVUKO CHA MV MAFANIKO NA KUZINDUA MRADI WA NYUMBA ZA NHC MKOANI MTWARA

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu
akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe  la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia  ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John  Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana.
 Sehemu kivuko hicho kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi  Mh.John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Jakaya  Kikwete kabla ya uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara  mapema leo mchana,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Fatma Salum Ali.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Fedha,Mh
Mwigulu Nchemba ambaye pia alihudhuria sherehe hizo fupi uzinduzi wa
kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
 Rais Kikwete akizindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.
  Rais Dkt.Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko cha Mv Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.Kivuko cha MV Mafanikio kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa ameambatana Waziri wa Ujenzi Dkt John
Pombe Magufuli mara baada kushuka kwenye kivuko cha Mv Mafanikio katika  kata ya Msanga  Mkuu-Mtwara vijijini mara baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya  Kikwete,kivuko hicho kina uwezo wa  kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa  kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
 Baadhi ya wananchi wa Msanga  Mkuu-Mtwara vijijini wakishangilia jambo mara baada ya kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa  kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3 kuzinduliwa na Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mchana mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa  kivuko cha MV Mafanikio
chenye uwezo wa  kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi  bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na  vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga  Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa  kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
 Bango la mradi huo
 Mkuruegenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na  wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na  NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,
 Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi  katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na  NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu  pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt
John  Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo. 
PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)