Pages

Proin Promotions Ltd yaendelea kufanya vizuri katika Maonyesho ya JAMAFEST jijini Nairobi Nchini Kenya

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Moses Mwanyilu akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika katika banda la Proin Promotions kwenye maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival yajulikanayo kama JAMAFEST yanayoendelea kufanyika jijini Nairobi Nchini Kenya.
 Baadhi ya watembeleaji wa maonyesho ya JAMAFEST yanayofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya wakiwa katika banda la kampuni ya Proin Promotions Ltd kwaajili ya kupata elimu kuhusiana na tasnia ya filamu Nchini Tanzania
Mmoja wa wateja aliyetembelea banda la Proin Promotions Ltd katika maonyesho ya JAMAFEST akifuatilia filamu ya Mpango Mbaya iliyokuwa ikionyesha kwenye runinga kama inavyoonekana kwenye picha.
 Baadhi ya wateja waliotembelea banda la Proin Promotions Ltd wakichagua filamu za Kitanzania kwaajili ya kununua kwenye maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival yanayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya katika viwanja vya KICC.
 Watembeleaji wakiangalia filamu zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Proin Promotions Ltd kwenye maonyesho ya jumuiya ya afrika mashariki JAMAFESTyanayoendelea kufanyika kwa siku ya tatu sasa katika viwanja vya KICC jijini Nairobi Nchini Kenya
 Banda la Proin Promotions Ltd linavyoonekana 
 Mmoja wa wateja akiangalia filamu zinazotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd katika maonyesho ya JAMAFEST yanayoendelea kufanyika jijini Nairobi Nchini Kenya
 
 Wakenya wakinunua filamu zinazotengenezwa na kampuni ya Proin Promotions Ltd katika maonyesho ya JAMAFEST.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)