Pages

NHIF YATOA “DARASA” KWA BLOGGERS WA TANZANIA KUHUSU UCHAGIAJI WA BIMA YA AFYA CHINI YA MPANGO WA “KIKOA”

 MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, akiwasilisha mada juu ya mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania, TBN, na kufanyika kwenye ukubmi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam, Agosti 13, 2015

NA K-VIS MEDIA MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Nchini Tanzania, NHIF, umekutana na wanachama wa chama cha waandishi wa habari wa mtandao (TBN), na kuwapa elimu juu ya mpango wa uchagiaji wa “KIKOA”, ambao unahusu watu binafsi walio kwenye vikundi.

Akitoa mada juu ya mpango huo,  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo anayesimamia mpango wa uchagiaji binafsi, (KIKOA),  Eugine Mikongoti, amesema, mfuko wa bima ya afya chini ya sheria ya kuanzishwa kwa mfuko huo, sheria namba 8 ya mwaka 1999, ni kusimamia upatikanaji wa huduma za kimatibabu kwa wananchi kwa utaratibu wa kuchagia kabla ya kuugua na kupata matibabu kupitia Hospitali za Serikali, Madhehebu ya dini, zan Binafsi na Maduka ya Dawa ambayo yamesajiliwa.

Alisema, mwanachama  wa KIKOA atachangia shilingi 76, 800/- kwa mwaka na atapatiwa kadi ya matibabu ya NHIF ambayo ataitumia kupata matibabu katika vituo zaidi ya 6,000 vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Pia alisema, Mwanachama wa KIKOA anayo fursa ya kuwaingiza mwenza wake na nafasi nne kwa ajili ya watoto (miaka 18 hadi 21) kama bado wanasoma na wazazi wake na wazazi wa mwenza wake, kwa utaratibu ule ule ya kuwalipia kila mmoja shilingi 76,800/- kwa mwaka kwa kila mmoja
 Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya Tanzania, NHIF, Rehami Athumani, akifungua warsha hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TBN, Khadija Kalili
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo, wakifuatilia kwa makini
 Rehani Athumani
 Bloggers kutoka Bagamoyo
Bloggers wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa

Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033 Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)