Selemani Rashidi, Namba msaada kwa yeyote anisaidie niweze kufanyiwa matibabu kwa kinyama kilicho jitokeza kichwani mwangu toka nilipo zaliwa.
Selemani Rashidi, anapoishi na mama yake mzazi
Selemani Rashidi (kushoto), akiwa na mama yake mzazi pichani, ambaye alisimulia mkasa mzima wa mwanaye, alizaliwa akiwa mzima na baada ya kuzaliwa alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa Degedege na alimpeleka kwa mganga wa kienyeji na kupona matatizo hayo na ndipo kikaota kipele kichwani cheusi na kikawa kinakuwa na kushikana na sikio, kutokuwa na uwezo wa kipesa hakuweza mpeleka popote, Baba yake yapata Miaka kumi na tano toka afariki na ukizingatia ni pesa inayo hitajika, hayo yalisemwa na mama yake mzazi ambaye anaitwa Zamda Kibosha, wakiwa wamekaa kwao maeneo ya kitongoji cha Lugongoni, (A) Kataa ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma, Mama yake anasema mwanaye baada ya kuota kinyama hicho, kauli kutoka ni kwa shida, akijibu maramoja harudii tena kuongea na chooni anakwenda mwenyewe na kula anakula kama kawaida, mama anaomba kwa mtu yoyote mwenye kuona na kusia anaomba msaada wa hali na mali ili mwanaye apate matibabu, kwa mawasiliano mwenye chochote kitumwe kwenye namba 0687946492, Mariam Hamza Thabiti, Nguruka kigoma. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)