Klabu ya Manchester United imekuwa miongoni mwa klabu ambazo zimetambulisha jei zao leo zitakazotumiwa kwa ajili ya msimu ujao. Klabu hiyo imevunja rekodi kwa kuwa ni klabu inayoingiza kipato kikubwa cha pesa duniani kutokana na utengezaji wa jezi .
Baada ya miaka 13 ya matumizi ya jezi za Nike, Manchester United sasa imeamua kuzindua jezi mpya zitakazotumika katika msimu wa 2015/2016. Man United watatumia jezi zitakazokuwa zinatengenezwa na Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas ya nchini Ujerumani.
Man United wamesaini mkataba wa miaka 10 na kampuni ya hiyo ya Adidas, mkataba wenye thamani ya pound milioni 750 na sasa wataanza kutumia jezi za kampuni hiyo.
Wakongwe hao (Adidas) wa kutengeneza vifaa vya michezo wanaamini wanaweza kutengeneza kiasi cha pauni bilioni 1.5 kutokana na mauzo ya jezi za Man U kwa muda wa miaka 10 ijayo.
Mkataba huo kati ya Manchester United na Adidas ni mkataba mnono zaidi kwa klabu hiyo ukilinganisha mikataba ya klabu nyingine ambazo zinatengenezewa jezi na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na klabu Bayern Munich (pauni milioni 645) na Chelsea (pauni milioni 300).
Jezi hizo mpya zitakuwa na muonekano kama ule wa zamani enzi za Ryan Giggs zikiwa na shingo ya V yenye rangi nyeupe na michirizi mitatu kwenye mikono yake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)