Majaji wa Shindano la TMT wakiwa ndani ya Mjengo wa TMT kwaajili ya kuwatembelea washiriki waliobaki mjengoni
Washiriki wa Shindano la TMT 2015 wakipitia muswada yaani script kabla ya kuingia kazi kwaajili ya kushoot filamu fupi
Washiriki wakiwasikiliza majaji kwa makini
Katika maandalizi ya short film wiki hii washiriki
wamepata wageni katika nyumba yao kule Masaki,wageni hao ni Majaji wa shindano
la Tanzania Movie Talents TMT 2015 Jaji
Mkuu Roy Sarungi,Jaji Monalisa,Jaji Rich Rich Single Mtambalike.
Majaji hao walipata wasaha wa kuzungumza na
washiriki wa TMT 2015 kwa kuwapa ushauri jinsi ya kufanikiwa katika maisha yao
kwa kuwa wenye nidhamu na wanyenyekevu katika sanaa bila kutaka kukumbilia
mafanikio,kuwa wabunifu watakapotoka kwenye mashindano ya TMT kwa kusema kidogo
walichokipata ni shule au mtaji tosha wa kuendeleza sanaa yako kama ajira.
Rich Rich au Single na Mtambalike na Monalisa
wakizungumza nao walisema wao miaka ya nyuma wakati wanaanza sanaa katika
vikundi kabla ya kuanza kuonekana ITV miaka ya nyuma walipitia wakati mgumu
sana kwa kutembea umbali mrefu kufuata sanaa au kushinda njaa ikiwa ni sehemu
ya kutafuta kitu wanachopenda,mwisho wa siku leo wameweza kufika hapa walipo na
kuwa wasanii wakumbwa nchi,walisema Rich Rich na Monalisa.
Washiriki waliongia katika
jua la utosi (Danger zone)kwa wiki hii ni Nadhifa Haruna, Mohamed Massanga,
Sadam Nawanda, Naomi Chuwa, Catherine Nicholaus na Rachel Michael
Mpigie
kura Mshiriki umpendae ili kutoka katika jua la utosi (Danger zone) aendelee
kubaki katika mashindano ya TMT 2015 na kumpa nafasi zaidi ya kushinda milioni
50. Andika TMT acha nafasi, namba ya mshiriki kisha tuma kwenda 0784367738.
Nadhifa
Haruna 01,Aisha Katabazi 02,Kalombo Amboni 04,Dennis Laswai 05,Tomluck Stephan
Shukuru 06,Catherine Nicholaus 07,Titus Maridhia 08,Daniel Lufingo
Jackson
Sakumi 12,Naomi Chuwa13,Sadam Nawanda 14,Mohamed Massanga 15,Saidi Bakari
Mbelemba16,Rachel Michael 17.
Usikose
kutazama kipindi cha TMT kinachoruka kila Jumapili saa 3:30 usiku,marudio
Alhamis saa 5:30 usiku na Jumamosi saa 7:00 mchana pekee!
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)