Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka balozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ambae ameingizwa mjini na muuandaaji wa shindano hilo
Muandaji wa shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015,Jackline Chuwa adaiwa kuingia mitini na fedha za zawadi za warembo na malipo kwa watu aliofanya nao kazi kufanikisha shindano hilo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya familia ya mshindi wa shindano hilo zinasema kuwa vikao vya mara kwa mara hufanyika kupanga mkakati wa kuvamia ofisi za BASATA kujua hatma ya binti yao Yolanda shayo.
ILIKUAJE:
Wakati wa kutangaza matokeo ya ushindi siku ya fainali za mashindano hayo usiku wa julai 24,mshindi alikabidhiwa Televisheni kama zawadi na kiasi cha pesa kilichoadiwa kutolewa na mdhamini mkuu ambae ni Coca cola.
Cha kustaajabisha muandaji huyo alienda ofisi za kampuni hiyo na kuchukua kiasi hiko cha fedha ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza lakini mpaka leo mrembo huyo anahaha kupata zawadi yake.
Yolanda aliamua kufunga safari mpaka ofisi za Bonite Bottles na kuwauliza wahusika kuhusu zawadi yake na alijibiwa kuwa muandaji huyo alishakabidhiwa fedha hizo siku nyingi.
Mrembo huyo alichukua hatua nyingine ya kumpigia simu Jackline na kumuulizia kuhusu zawadi yake ya fedha taslimu alioadiwa jukwaani na wadhamini wakuu,chakushangaza muandaaji huyo alitoa kauli ya kumvunja moyo kwa maana hatoipata kabisa kwa kisingizio eti hakupata faida.
FAMILIA YA YOLANDA:
Familia ya mrembo huyo imechukizwa na kitendo cha muandaaji huyo kwa kuingia mitini na zawadi ya binti yao na bila kumkabidhi mikononi mwa kampuni hiyo ambapo ilitoka ahadi kuwa atakuwa balozi wa kampuni hiyo kufanya kazi mbalimbali kama balozi wa kinywaji hiko mkoani humo.
Wazazi wa mrembo huyo wamedhamilia kutinga ofisi za BASATA kufatilia mkataba wa bitni yao kutokana hali ya sintofahamu kuendela toka binti yao atawazwe kuwa mshindi mnamo julai 24.
Pia wanafamilia wametoa shutuma nzito kwa shindano hilo wakihoji ni kwanini msanii wa bongo flava anapewa milioni 25 kutumbuiza wakati binti yao ambae ndiye mshindi anambulia zawadi ya televisheni pekee.
WASHIRIKI WENGINE:
Hali ni tata pia kwa washiriki wa walioingia tano bora hasa namba nne ambae alizawadiwa laki nne na mapazia kutoka kampuni ya Mapazia house lakini chakushangaza muandaji huyo aliingia mitini na fedha hizo na kumuacha mrembo akirudi nyumbani na mapazia tu.
Mrembo huyo Willice Donard amelalamikia kitendo cha muandaji huyo kumjibu majibu ya dharau pale alipompigia simu kuulizia zawadi yake.
Habari zinasema kuwa mrembo alieshika namba tano,Femy Lema alipokonywa nusu ya kiasi cha fedha alichokabidhiwa jukwaani ikiwa ni zawadi ya kuingia tano bora.
KAMATI YA MAANDALIZI:
Hali si shwali kwa upande wa kamati,habari za uhakika toka kwa watu walioshiriki kumpa sapoti muandaaji huyo zikizadai kuwa amewaingiza chaka na kuwazulumu haki yao ya malipo,mpaka sasa hawajui fedha zao watazipataje.
KAULI ZA MUANDAAJI:
Kauli za muandaji zilizojaa dharau na kejeli kwa watu wanaodai haki zao ndizo zilizowapandisha hasira na kufanya baadhi ya watu kutoboa ukweli huu kwani amekuwa akiwaambia anaenidai aende mahakamani huko ndiko haki ya mtu hupatikana kwa kisingizio eti amesomea sheria.
KUMBUKUMBU ZAKE:
Kumbukumbu za muandaaji huyu zinaonesha ni mtu ambae anapenda mambo ya ujanja-ujanja na kujipatia faida kubwa kupitia majina ya watu kama alivyotaka kumtumia Zari Hassan kuvuta watu wengi kuingia katika tamasha lake na angali hakuwa na mkataba wowote na Zari.
Kitendo hiko kilimfanya Diamond Platnumz kutaka kususia na kuandika maneno makali katika ukurasa wake wa instagram,kitu kilichompelekea kutozwa faini na uongozi wa Zari.
BASATA:
Wito umetolewa kwa balaza la sanaa kuwa makini kwa kutoa vibali kwa waandaji wasio na uhakika na shughuli wanazofanya kama ilivyotokea kwenye hili shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015.
Tunaamini dhamira ya shindano hili ni nzuri na lina manufaa kwa jamii kuhusiana na utalii,utamaduni na kazi za kijamii,shindano hili lina faida ila tatizo liko kwa muandaaji mwenyewe kana kwamba hana malengo na shindano hilo.
Lawama za pekee ziende kwa Basata kwani shindano hili lilipelekwa kienyeji bila usimamizi wowote kama ilivyo kwa mashindano mengine makubwa,isitoshe kanuni na taratibu hazikufuatwa mwanzo mwisho ndiyo maana leo tunapata malalamiko ya mshindi Yolanda shayo kuingizwa mitini zawadi na mkataba wake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)