Pages

Fainali ya TMT kufanyika tarehe 22 August ndani ya Makumbusho ya Taifa Posta

Shindano la kuibua na Kusaka Vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limedumu kwa takribani Miezi Minne hatimaye shindano hilo linakaribia kufika tamati mnamo tarehe 22 August 2015 huku Mshindi Mmoja Akiondoka Na Kitita Cha Shilingi Milioni Hamsini Za Kitanzania. Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.

Shindano la TMT lilianza mapema mwezi wa Nne kwa kutafuta vipaji katika Kanda ya Ziwa ambapo usaili ulifanyika Mkoani Mwanza na kuhitimishwa Kanda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam kwa kupatikana Jumla ya Washindi 20 kutoka Kanda sita za Tanzania

Washindi wa kanda sita walipata fursa ya kuingia ndani ya mjengo wa TMT huku wakipatiwa mafunzo ya sanaa kutoka kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam huku mchujo ukiendelea na kupelekea kila wiki Washiriki wawili kuaga shindano, takribani wiki tano jumla ya washiriki 10 waliweza kuaga shindano hili ambalo limefikia hatua ya kuwapata washiriki 10 waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora huku wakingojea fainali itakayotoa mshindi wa kitita cha shilingi milioni hamsini za kitanzania

Mpaka sasa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora wanaendelea na kujifua Kwaajili ya fainali ambayo imebaki wiki moja tu kwa fainali hiyo kuliteka jiji la Dar huku hofu na presha zikiwapata Washiriki hao.

Fainali ya TMT itafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa makumbusho ya taifa karibu na Chuo cha IFM kwa viingilio vya shilingi Elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa viti vya kawaida.

TMT 2015 inapigwa tafu na Precious Air, Cam gas, ITV na Radio One, Global Publishers, I-View Studio, Paisha na Hussein Pamba Kali

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)