Wakazi wa Dar es salaam Kupata matibabu yatakayotolewa na
wataalamu kutoka Hospitali za Apollo.
Watanzania
wanashauriwa kuitumia fursa hii ya kipekee ya ziara ya kitabibu itakayofanywa
na madaktari kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad. Kwa miaka mingi, watanzania wameshindwa kupata
matibabu sahihi nchini kitendo ambacho kimewasababishia kusafiri nje ya nchi
kupata matibabu sahihi ya mfumo wa fahamu, uti wa mgongo, figo pamoja na magonjwa
yanayohusiana na mfumo wa mkojo. Nia na
madhumuni ya ziara ya madaktari na washauri hawa kutoka Hospitali za Apollo
nchini Tanzania ni kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata vipimo sahihi kwa
gharama nafuu. Madaktari bingwa watatu wanao ongoza katika Hospitali za Apollo
watafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Hindu Mandal kutoa
huduma za kimataifa kwa watanzania.
Wagonjwa
wanaougua magonjwa yanayohusiana na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, figo na
magonjwa ya kibofu cha mkojo, wanashauriwa kuhudhuria na kushiriki tukio hili
la kipekee. Madaktari watatembelea wagonjwa, kufuatilia historia za wagonjwa na
kuwashauri matibabu sahihi kutokana na ripoti za matibabu na vipimo.
Daktari wa
kwanza atakayeshiriki katika kutoa ushauri na matibabu ni Dkt. Alok Ranjan
ambaye ni mtaalamu katika upasuaji mishipa ya fahamu na uti wa mgongo katika
Hospitali za Apollo mjini Hyderabad. Atapatikana siku ya Jumatatu ya tarehe 27
Julai na tarehe 28 Julai kati ya saa 03 asubuhi
na 11 jioni kwa tarehe hizo mbili katika Hospitali ya Hindu Mandal
jijini Dar es salaam. Dkt. Alon Ranjan
ni mtaalamu anayeongoza katika upausaji wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo
kwa zaidi ya miaka 20 kwa kufanya upasuaji mgumu wa mishipa. Dkt. Alok Ranjan
ameongoza timu yake kufanya pasuaji mbali
mbali za mishipa ya fahamu zaidi ya 1,000
kama vile upasuaji mdogo wa mtindio wa ubongo, upasuaji wenye madhara
madogo wa uti wa mgongo, upasuaji mgumu wa uti wa mgongo, na upasuaji kwa
kutumia kifaa maalumu cha kuangalia uti wa mgongo na ubongo.
Kliniki ya
ushauri na tiba ya pili imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 31 Julai
na 01 Agosti katika Hospitali ya Hindu Mandal ya Dar es salaam. Wagonjwa
watapata fursa ya kupata ushauri na tiba kutoka kwa Dkt. Rajagopal ambaye ni
mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi na Dkt. Sanjay Maitra ambaye ni mtaalamu
wa figo kati ya saa 3 asubuhi na saa 11 Jioni kwa siku za Ijumaa na Jumamosi.
Huduma hizi za ushauri na tiba, zitatolewa kwa gharama nafuu.
Dkt.
Rajagopal amebobea katika magonjwa ya mfumo
wa mkojo na mfumo wa uzazi kwa wanaume. Amekuwa mshauri mwandamizi wa tiba wa
magonjwa ya vina vya uzazi katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad tangu
mwaka 1994.
Dkt Sanjay
Maitra amebobea katika huduma na tiba za magonjwa ya figo na magonjwa yanayo
shabihiana na haya. Kwa kawaida
madaktari hawa hutibu magonjwa sugu ya figo, uvimbe katika figo, figo
zilizoshindwa kufanya kazi na jiwe figo ikiwa ni pamoja na kuelimisha juu ya
masuala mbali mbali ya upandikizaji wa figo na usafishaji. Dkt. Sanjay Maitra ana uzoefu wa miaka mingi
katika tiba ya figo na alimaliza masomo yake ya utaalamu wa magonjwa ya figo
kutoka katika chuo cha AIIMS mjini New Delhi. Dkt Sanjay Maitra pia amekuwa
akitoa mafunzo ya upandikizaji wa figo kutoka katika miili iliyo kufa na iliyo
hai, huduma muhimu za ubadilishaji wa figo, usimamizi wa mda mrefu wa
usafishaji wa figo kwa wagonjwa.
Hii siyo mara
ya kwanza kwa madaktari hawa kutembelea Dar es salaam. Ushirikiano huu endelevu na Hospitali ya
Hindu Mandal unathibitisha dhamira ya Hospitali za Apollo katika kutoa huduma
bora za afya na nia thabiti ya kuendeleza mahusiano na Tanzania ambayo
yameazishwa kwa Zaidi ya muongo mmoja.
Katika siku
hizi ambazo madaktari hawa watatoa tiba na ushauri, Dkt. Alok Ranjan, Dkt. Sanjay Maitra na Dkt.
Rajagopal watakuwa wanapitia kujua hali za wagonjwa ambao waliwahi kutibiwa
mjini Hyderabad au ambao walitibiwa kipindi ambacho madaktari hawa walitembelea
Dar es salaam mara ya mwisho. Katika
kipindi hiki, madaktari hawa watafanya mahojiano na wagonjwa kujua historia ya
ugonjwa wao, kuwafanyia vipimo, kujadili sababu zinazoweza kuwa vyanzo vya
ugonjwa wao, matibabu yanayoweza kutolewa inchini, kuwaandikia wagonjwa dawa na
kufanya mipango ya vipimo au kupendekeza matibabu ya ziada. Kwa baadhi ya wagonjwa, kutegemeana na ukubwa
wa tatizo la mgonjwa na hali yake, wagonjwa wanaweza kushauriwa kutafuta
matibabu zaidi nje ya nchi kwa matibabu ambayo hayawezi kufanyika nchini
Tanzania. Katika kipindi hiki, wagonjwa
watajadiliana na madaktari majibu ya vipimo au ripoti za vipimo vilivyofanyika
hivi karibuni. Kliniki hii ni fursa ya
kipekee kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yahusianayo na uti wa mgongo,
mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo na ambao wanahitaji
ushauri mbadala au wale ambao hawawezi kumudu gharama za kupata matibabu nje ya
nchi.
Ndugu Radhey
Mohan, Makamu wa Raisi wa Maendeleo ya Kimataifa Kibiashara anadhamini kliniki
hizi kwa kushirikiana na Hospitali ya Hindu Mandal.
Wagonjwa
wanahamasishwa kufaidika na kufursa hii na wanashauriwa kujiandikisha kupata
ahadi ya kuwaona madaktari hawa katika
Hospitali ya Hindu Mandal kwa kupiga simu nambari +255 22 211 4991-4
Kuhusu Apollo
Mnamo mwaka
1983, Dkt. Prathap C Reddy, mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali
ya kwanza ya ushirika nchini India, Apollo Hospitals Chennai. Kwa miaka mingi,
Hospitali za Apollo zimeweza kukuwa kufikia kuwa moja ya shirika kubwa la afya
barani Asia likiwa na uwezo wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50,
zaidi ya maduka 1350 ya dawa na zaidi ya
kliniki za uchunguzi 100. Pia
Hospitali za Apollo hutoa huduma za
matibabu kwa utaratibu wa kibiashara,
huduma za bima za afya na kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo la kufanya
tafiti za magonjwa ya milipuko, seli shina za mwili na maumbile. Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji
linaloongezeka katika utoaji wa huduma
za hali ya juu, Hospitali za Apollo zina jumla ya vyuo 11 vya madaktari pamoja
na wauguzi. Mafanikio haya yamezifaidisha Hospitali za Apollo kupata tuzo mbali
mbali, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India
pamoja na kutambulika na tume ya pamoja ya kimataifa (Hospitali saba za Apollo
zinatambuliwa na kutunukiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika heshima
nadra, serikali ya India ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa
Hospitali za Apollo, ikiwa ni shirika la kwanza la afya kupata heshima
hiyo. Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo
Dkt. Prathap C Reddy, alitunukiwa tuzo ya heshima ya ‘Padma Vibhushan’ mnamo
mwaka 2010. Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea
kuboresha uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kliniki za kimataifa
na maendeleo ya teknologia. Hospitali
zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimataifa katika huduma za kitabibu pamoja
na utafiti.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)