Mbabazi ametangaza atawania urais kama mgombea huru
Waziri mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani.
Mbabazi ametangaza hilo muda mchache uliopita akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala.
''kamwe sitatoka NRM''.
''Lakini sitaweza kugombea urais katika tikiti ya chama hicho cha NRM ilihali vipengee vingi tu vya vya chama vinakiuka katiba ya nchi''.
'' sitawania urais kwa tikiti ya NRM lakini wakati wa uchaguzi nitawania urais'
''kama mwanzilishi wa chama ,wakili na mwananchi Mzalendo,sitajiingiza katika maswala yanayokiuka sheria''
NRM sharti ijipige msasa''
Tangazo hilo la Mbabazi limetokea baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kuwa atarejesha fomu zake za kuwania uwenyekiti wa chama tawala NRM leo.
Mwenyekiti wa jopo la kuchagua viongozi wa chama hicho bwana Tanga Odoi alikuwa ametanga ijumaa tarehe 31 (leo) kuwa siku ya mwisho ye kurejesha fomu za uwaniaji nyadhfa za chama hicho.
Mbabazi anasemekana kuwa alitembelea makao makuu ya chama tarehe 16 akikusudia kuwasilisha ombi lake lakini akakurupuka akidai kuwa gharama ya juu iliyowekwa kwa wagombea itawanyima maskini uwezo wa kuwania nyadhfa katika chama hicho.
Mbabazi alikuwa ameahidi kumpinga rais Museveni kama mwenyekiti wa chama na hivyo mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Mpinzani wake rais Museveni anatarajiwa kurejesha fomu zake mwendo wa saa sita adhuhuri.
katika makao makuu ya chama, wafuasi wake wamemiminika wakiwa wamevalia rangi za chama wakiimba nyimbo za kumsifu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)