Jaji Msumi (katikati), akiwa na wenzake akisikiliza shauri hilo.
Na Dotto Mwaibale
KAMANDA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya ya Mkuranga, Damas Pasalau, amemkingia kifua aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya Mkuranga Sipora Liana kwa tuhuma zinazomkabili katika Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa katika vikao vya baraza a maadili vilivyoanza jana jijini Dar es Salaam, Sipora ambaye kwa sasa Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha anakabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili.
Inadaiwa kuwa mnamo mwaka 2009/2010 Sipora alimchukulia hatua za kinidhamu bila sababu za msingi kwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika Wilaya ya Mkuranga Dk. Fransis Mallya kinyume na sheria ya maadili ya utumishi wa umma.
Pasalaus alitoa utetezi kwa muda wa dakika 30 ambapo kati ya hizo 10 alizitumia kutoa utetezi wakati akiulizwa maswali na Mwanasheria wa Serikali Getrude Cyriacus.
Pasalau ambaye mara kwa mara alibanwa na mwanasheria huyo kwaajiri ya kutoa ushahidi sahihi aliendelea kumtetea huku akitoa mifano mbalimbali na utendaji kazi wake uliofanyika katika Wilaya aliyotoka Sipora huku akidai kuwa ni kitendo hichop ni chuki binafsi hivyo zisiruhusiwe kushika nafasi kwenye mali za umma.
Wakati akitoa ushahidi huo alimtaka Jaji Hamis Msumi kutenda haki na kudai kuwa Mkurugenzi huyo hana kosa bali ni hujuma za baadhi ya watu ambao walikuwa kwa maslahi yao binafsi katika ofisi za Manispaa hiyo.
Alisema awali katika Manispaa hiyo kulikuwa na msuguano kati ya Madiwani, watumishi wa umma na wakurugenzi jambo ambalo baada ya kufanyika kwa uchunguzi na taasisi hiyo ilibainika uwepo wa ubadhilifu wa mali za umma.
"Baada ya Sipora kuwasili katika halmashauri hiyo ambapo katika utendaji kazi wake mzuri watu wengi hawakumpenda kwani wengi wao walikuwa wakifanya shughuli zao kwa maslahi binafsi," alisema.
Alidai baada ya Mkurugenzi huyo kufika na kuonekana utendaji wake unawabana baadhi ya watu akiwemo Mallya na wenzie waliunda kundi ambalo lilikuwa ni kwaajili ya kupambana nae.
"Watu hawa walitumia vyombo vya udhibiti wa maadili kutunga hoja za uwongo ili kuweza kufanikisha malengo yao.
" Ila kiukweli mwenyekiti huyu mama amethubutu na ameweza kulingana na hali ya mazingira yaliyoko katika halmashauri ile kwatu watendaji wengi hawakupenda watu wa aina hii," alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu tatizo lililotokea hadi hatua za kusimamishwa kazi zilipotokea alidai kuwa baada ya Mkurugenzi huyo kuwasili katika halmashauri hiyo alianza kufuatilia idara ya Mallya katika kukamilisha miradi ya Mabwawa ya Mkwalia pamoja na ununuzi wa vitotozi visivyofanyakazi na kuweka mashamba hewa ambapo hakuwa amefanya kazi yeyote.
Hata hivyo shauri hilo liliahirishwa kutokana na anaedaiwa kuwa ni mlalamikiwa Sipora, kutofika na mashahidi wake kama alivyowasilisha idadi yao katika baraza la hilo.
Akihairisha kikao cha baraza hilo, Jaji Msumi alisema shauri hilo litasikilizwa hadi pale itakapotolewa hati maalum ya wito kwa mashahidi wa Mkurugenzi huyo.
.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)