Pages

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU NA TAARIFA ZISIZO NA UKWELI DHIDI YA WASHIRIKI WA TMT 2015

Picha ya Post iliyopostiwa na Kijana ajulikanae kama Raffayel Mombury.

Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ni waandaaji na waendeshaji wa shindano la Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo linaendelea kufanyika huku washiriki watano Wakiwa washaenguliwa katika shindano hilo Kutokana na Kutokupata kura za kutosha kutoka kwa watazamaji wa Kipindi hiko mahiri kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV siku ya jumapili saa tatu na nusu usiku.

Proin Promotions tunasikitika kusema kuwa kuna habari ambazo sio za kweli ambazo zimepostiwa katika ukurasa wa facebook wa kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Raffayel Mombury ambae amepost taarifa hiyo yenye kichwa cha Habari "WASHIRIKI WA TMT 2015 WAFUMANIWA WAKINGONOKA" kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu, Sisi kama Proin Promotions ltd tunapenda kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na sura hizo hatuzitambui na wala sura zinazoonekana katika post hiyo sio za washiriki wetu wa TMT 2015 na hazijawahi kuwa. 

Kutokana na post hiyo ambayo yenye mlengo wa kuichafua Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa shindano pamoja na mradi mzima wa TMT ambao unaaminika Tanzania Nzima na Nje ya Tanzania tumepata usumbufu mwingi kutoka kwa wapenzi wa Shindano hilo pamoja na wazazi wa Washiriki waliobakia. Tunapenda kusema kuwa kiukweli taarifa hizo zimetuletea usumbufu mkubwa sana na kupelekea kuvunja imani kwa watazamaji wetu na wapenzi wa vipindi vyetu, Sisi kama Proin Promotions tunawaomba Watanzania na Wapenzi wa TMT  kuzipuuza taarifa hizo na hakuna kitu kama hiko kwasababu Nyumba wanayoishi washiriki wa TMT 2015 imezingatia maadili makubwa na kuwepo kwa usimamizi wa matron katika kambi hiyo.

Proin promotions tunasema kutokana na taarifa hizi kutokuwa na ukweli wowote tunaahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu huyu aliyesambaza taarifa hizi za uongo na zilizotuletea usumbufu mkubwa sana katika jamii inayofuatilia shindano hili na kupelekea kupoteza imani kwa jamii.

Imetolewa na
Idara ya Mahusiano ya Umma
Proin Promotions Ltd

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)