Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick akiosha pikipiki ya Blogger Mroki Mroki 'Father Kidevu' (kushoto kwake) wakati wa harambee kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiosha pikipiki hiyo baada ya kuzidi dau na kufanya jumla ya shilingi 150,000/= kupatikana kwa kuosha pikipiki hiyo.
Mdauhuyu nae alikuja na Baiskeli yake kwaajili ya kushiriki zoezi hilo na baikeli hiyo ilichangiwa 40,000/= ili ioshwe. Daudi Mambya akiosha baiskeli hiyo na kuchangia waandishi.
Kama vile haitoshi nayo Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia walifanikisha kuchangia kiasi cha shilingi 1,350,000/= kufuatia kuguswa kwa namna moja nyingine kwa kampeni hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani.
Mbali ya fedha hizo kupatikana pia walijitokeza watu mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER,ambalo kwa kiasi kikubwa bado linahitaji kuongeza hamasa zaidi ili wadau wazidi kujitokeza na kuchangia.
Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha,huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mh Meck Sadick.
Aidha Miongoni mwa taasisi zilizochangia harambee hiyo ni Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Benki ya Posta Tanzania (TPB), Redio 5 ya Arusha, TANAPA, NSSF, NHIF, na wengine wengi pamoja na baadhi ya wabunge, Wakuu wa Wilaya na watu binafsi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiendelea Kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika Media Car Wash for Cancer. Ikiwa ni kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa
afya zao.
Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi zima la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)