NJAMA ZA MAKABURU KUMG'OA MKURUGENZI WA KONYAGI MGWASSA ZAGUNDULIKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NJAMA ZA MAKABURU KUMG'OA MKURUGENZI WA KONYAGI MGWASSA ZAGUNDULIKA

 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), maarufu kwa jina la Konyagi . David Mgwassa Kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) Jijini Dar es Salaam.Mwandishi Wetu

MKAKATI wa kumng'oa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi (TDL) David Mgwassa umebainika kutokana na kuwepo kwa njama zinazoendeshwa kwa siri na makaburu.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kiongozi huyo amekuwa akipigwa vita kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mafanikio yanayopatikana chini ya uongozi wake.

Makaburu hao wamekuwa wakifanya njama mbalimbali za kumng'oa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutaka kushika wadhifa wa mkurugenzi huyo kwa kutoa taarifa ambazo si za kweli kwa uongozi wa ngazi za juu nchini Afrika Kusini na Uingereza.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa kiongozi huyo ametakiwa kukabidhi ofisi ifikapo Julai 30, mwaka huu.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa tayari taarifa za kuondolewa kwa kiongozi huyo zimezagaa katika viwanda vya TDL na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) pia tangazo la kumbadilisha limetolewa kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kutangaza Kenya na Uganga.

Kutokana na taarifa hizo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TDL wameazimia kugoma ili kushinikiza mkurugenzi huyo kuendelea na madaraka yake.

"Tumesikia taarifa kuwa mkurugenzi wetu anaondolewa madarakani kwani tumeshangazwa sana kutokana na kuishi naye vizuri na kupatikana kwa mafanikio mengi tangu ashike wadhifa huo na pia ameboresha maisha yetu kwa kutuongezea mishahara," alisema mfanyakazi mmoja ambaye hakutaja jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa wafanyakazi.

Hata hivyo kuna taarifa kuwa Bw. Michael Benjamin anatarajia kushika wadhifa wa Bw. Mgwassa.

Mtandao huu ulimtafuta Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Steve Kilindo ili kuzungumzia taarifa hilo alikiri kuwepo kwa mabadiliko hayo lakini hana taarifa zaidi kuhusiana na sakata hilo.

"Kweli kuna mabadiliko hayo ya uongozi lakini taarifa za ndani sina," alisema.
                         Mike Benjamin kutoka Afrika Kusini anayetarajia kurithi cheo hicho

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages