Chaula akiagana na mshindi mzee Nkwera |
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Antonia Choya akimkabidhi hati ya shukrani mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto)
Mjumbe wa mkutano huo Bw Choya akipiga kura
Wajumbe wakishiriki kupiga kura
Wajumbe wakishiriki kupiga kura
Mgombe Chaula akishukuru kwa kushindwa
Injinia Chaula akimpongeza mshindi mzee Nkwera
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akipiga kura kumchangua mjumbe wa NEC Ludewa
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Deo Filikunjombe akikabidhiwa hati ya shukrani ya kushiriki mbio za Mwenge toka kwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Antonia Choya ,hati iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe
Na MatukiodaimaBlog
MBIO
za ubunge jimbo la Ludewa mkoani Njombe zimeishia hewani kwa
mtangaza nia wa wanafasi hiyo Injinia Zephania Chaula baada ya
kuambilia kura 11 pekee katika nafasi ya mjumbe wa Halmashauri kuu (
NEC) Taifa kutoka wilaya ya Ludewa aliyokuwa akiwania dhidi ya katibu
msaidizi wa mbunge wa jimbo la Ludewa Hilaly Nkwera aliyeibuka
mshindi kwa kupata kura 138 kati ya kura zote halali 151 zilizopigwa .
Huku mgombea huyo aliyeshindwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa NEC Injinia Chaula akiapa kutogombea tena nafasi hiyo kwa
madai kuwa ni mara ya pili sasa anashindwa vibaya katika mchakato
wa kuwania nafasi hiyo ambapo awali alishindwa mgombea wa darasa la
saba marehemu Elizabeth Haule .
Uchaguzi
huo mdogo wa kuziba nafasi ya mjumbe wa NEC iliyoachwa wazi na
aliyekuwa mjumbe wa nafasi hiyo Elizabeth Haule aliyefariki dunia
mapema mwaka huu ,ulifanyika mwishoni mwa wiki hii kwa
kuwashirikisha wagombea hao wawili kabla ya mgombea mwingine ambae
ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuandika barua ya
kujitoa katika kinyang'anyiro hicho akiwapisha wagombea hao
wachuane kutokana na yeye kudai kuwa atachukua fomu ya kugombea tena
ubunge wa jimbo hilo la Ludewa .
Akitangaza
matokeo hayo ya uchaguzi msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Lucas
Nyanda ambae ni katibu wa jumuiya ya wazizi wa CCM mkoa wa Njombe
,alisema kuwa jumla ya wajumbe waliopaswa kushiriki katika
uchaguzi huo ni 164 ila wajumbe halali walioshiriki ni 151 na kati
ya wajumbe hao kura 2 ziliharibika huku Injinia Chaula akipata kura
11 na mshindi wa nafasi hiyo Bw Nkwera akipata kura 138
Awali
mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Filikunjombe ambae alikuwa ni mmoja
kati ya wana CCM watatu ambao majina yao yalirejeshwa kuwania
nafasai hiyo alisema kuwa analazimika kujitoa katika nafasi hiyo
ili kupisha wanachama hao wawili ambao wamemzidi umri ili kuweza
kupambana na yeye ataendelea kuwa kuwatumikia wananchi wa Ludewa
katika nafasi ya ubunge pekee.
Akiwashukuru
wajumbe
kwa ushindi huo wa nafasi ya ujumbe wa NEC Bw Nkwera ambae
kitaaluma ni mwalimu na pia amepata kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa madiwani wa mkoa wa Njombe na Iringa
alisema kuwa
amefurahishwa na imani kubwa ambayo wana CCM wameionyesha kwake kwa
kumchagua kuwa mwakilishi wao katika vikao vya kitaifa .
Bw
Nkwera alisema wana CCM Ludewa waamini kuwa nafasi hiyo hawajakosea
kumpa na kamwe hatawaangusha kwani atahakikisha anawatumikia vema
katika vikao vya juu kwa kuanza na safari ya kumpata mgombea wa
nafasi ya Urais wa CCM ambae atakuwa ni chaguo la wana CCM wote wa
Ludewa .
Huku
Chaula mbali ya kuwashukuru kwa kura 11 alizopata bado alisema
kuwa hatakuwa tayari kuendelea kugombea tena kwani yawezekana kabisa
Mungu hajapenda yeye kuwa kiongozi wa kisiasa bali ametaka aendelee
kuwa mtaalam .
“Nasema haya
kutoka moyoni mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi na nakipenda chama change
hivyo naahidi sitagombea tena katika maisha yangu nafasi hii ya UNEC kutokana
na ukweli kuwa nahisi siasa inanikataa maana kila nikigombea nashindwa hivyo
ngoja nifanye kazi nyingine pia nampongeza sana mshindi Mzee Nkwera katika
utendaji wake ndani ya chama”,alisema Mhandisi Chaula.
Wakati
huo huo serikali ya mkoa wa Njombe kupitia mkuu wa mkoa wa Njombe
Dr Rehema Nchimbi imempongeza kwa kumpa hati ya shukrani mbunge wa
jimbo la Ludewa Bw Filikunjombe kwa ushiriki wake mkubwa katika
kufanikisha mbio za mwenge katika mkoa huo kwa kuwa mbunge pekee
kushiriki mbio za mwenge na kuchangia vizuri .
Akikabidhi hadi hiyo mbele ya wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu , mkuu wa
wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya aliweza kumtunuku hati hiyo ya heshima mbunge wa
jimbo la Ludewa Filikunjombe kwa kushiriki kimamirifu katika mbio za
mwenge wa Uhuru ndani ya mkoa wa Njombe.
Akitoa cheti
hicho Bw.Choya alisema kuwa kutokana na ushiriki alioufanya mh.Filikunjombe
katika mbio cha mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe na ofisi yake wameona
wampatie cheti cha heshima Filikunjombe kwani ni mbunge pekee aliyeshiriki
katika mbio hizo za Mwenge katika mkoa wa Njombe.
MWISHO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)