Pages

Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akabidhi soko jipya la SIMU 2000 kwa wafanyabiashara

Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akitoa maelekezo kwa  watendaji wa soko hilo  wakati akagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.
Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hio wakikagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.


MSTAHIKI Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni. 
Mstahiki  Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa. 
Meya  Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya Kinondoni tu, na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao. 
“Tumeamua kulifanya soko hili ili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda. 
 Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)