JovagoTanzania wapunguza bei za mahotelini mpaka 53% Jijini Dar es Salaam .
Kama ilivyokawaida , kila mwaka
Saba saba ni sikukuu ya Kibiashara ya kimataifa inayofanyika kila mwaka jijini
Dar es Salaam kuanzia tarehe 28Juni –mpaka tarehe 8 Julai , ambapo siku ya
tarehe saba mwezi wa saba( 7 Julai) ni siku ya kilele cha siku kuu hiyo.
Siku kuu hii ya 39 ya mwaka 2015,
inakadiriwa kuhudhuriwa na nchi 18, na kuwa na idadi ya watu wapatao 1800 wasio
raia wa Kitanzania wanaohusika katika kufanya maonyesho. Siku kuu hii imekuwa
ni chambo cha kutambulisha bidhaa na huduma z
Kulingana na wageni wengi kutoka
ndani na nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo na uhudhuriaji wa sekta mbali
mbali za kiserikali na watu binafsi , Jovago
Tanzania
inapendelea kuweka muongozo kwa wageni
wa maonyesho ya Saba Saba kwa
kuorodhesha hotel 3 bora za ndani ya Dar
es Salaam zilizo na usalama na kukuwekea punguzo la bei mpaka 53% ya malipo.
New
Avon Hotel, Ploti namba 975/149 mtaa
wa Aggrey na Jamhuri , Dar es Salaam .
Hoteli hii inafaa zaidi kama unapendelea kukaa katikati ya mitaa na maduka ya
kutosha , pia ipo karibu na uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere, mahali hapa panafaa zaidi kwa wageni wafanya biashara na
wanaopendelea kufanya tafiti za kibiashara katikati ya mji.
Blue
Pearl Hotel and Apartments, inakupa punguzo mpaka 44% kutegemea na idadi
ya vyumba, ipo katika barabara ya kuelekea Morogoro, eneo la Ubungo
Plaza, Dar es Salaam. Hoteli hii ina zaidi ya vyumba 31, na kuwapa wateja wake
mahala pa kupaki magari kwa usalama, pia inatoa huduma ya internet na sehemu za
kufanyia mazoezi, hakuna matatizo ya umeme na inahakikishia usalama kwa kila
mteja wake.
Denfrances Hotel, inakupa punguza mpaka 42%,
iko maeneo ya Sinza, karibu na barabara ya Shekilango, Dar es Salaam. Kila
chumba kina ulinzi wa kutosha, na inatoa huduma za chakula hapohapo kwa urahisi. hoteli inatoa huduma za kumbi za mikutano , ambapo inawafaa
zaidi watu wenye misafara ya Kibiashara.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)