Pages

Lowassa achukua fomu kugombea Urais Chadema

Lowassa akiwaonesha wanachama wa chama hicho fomu mara baada ya kukabidhiwa. Lowassa akiwaonesha wanachama wa chama hicho fomu mara baada ya kukabidhiwa.Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimkabidhi fomu za kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa katika hafla ya zoezi hilo lililofanyika leo. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimkabidhi fomu za kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa katika hafla ya zoezi hilo lililofanyika leo.Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimkabidhi fomu za kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa katika hafla ya zoezi hilo lililofanyika leo. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimkabidhi fomu za kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa katika hafla ya zoezi hilo lililofanyika leo.Lowassa akikabidhiwa fedha za mchango wa fomu na baadhi ya wanachama wa CHADEMA mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais. Lowassa akikabidhiwa fedha za mchango wa fomu na baadhi ya wanachama wa CHADEMA mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais.Lowassa akikabidhiwa fedha za mchango wa fomu na baadhi ya wanachama wa CHADEMA mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais. Lowassa akikabidhiwa fedha za mchango wa fomu na baadhi ya wanachama wa CHADEMA mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais.Lowassa akiwasili ofisi za Chadema kuchukua fomu ya kugombea urais. Lowassa akiwasili ofisi za Chadema kuchukua fomu ya kugombea urais.Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA. Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.

WAZIRI Mkuu mstaafu na mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo amechukua fomu za kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho. Lowassa ambaye msafara wake ulikuwa na wananchi wengi kiasi ambacho uliwashinda vijana wa ulinzi wa CHADEMA, aliwasili katika Makao Makuu ya chama hicho majira ya saa sita na nusu na kupokelewa na wanachama wengi waliokuwa wamejipanga pembeni mwa barabara ya mtaa zilizopo ofisi za chama hicho.

Akizungumza kabla ya mgombea huyo kukabidhiwa fomu, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu(Mb) alisema katiba ya Chadema na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamruhusu Lowassa kugombea urais endapo atapitishwa na chama hicho. Alisema Lowassa anaruhusiwa kuzunguka ili kujitambulisha kwa wananchi kwamba ameomba kugombea nafasi hiyo na wamuunge mkono.

Lissu alisema taarifa zinazotolewa kuwa chama hicho kimegawanyika baada ya kuingia Lowassa ni za uzushi na kuwataka WanaChadema na wananchi wazipuuze, kwani hakuna ukweli wowote wa suala hilo. Aliwataka viongozi wa Chadema pamoja na Lowassa kujipana ili kuhakikisha wanashinda viti vingi vya nafasi ya ubunge na cha urais ili waweze kuunda Serikali. Alisema wanatakiwa kushinda zaidi ya viti vya ubunge 133 ili kupata sifa kikatiba ya kuunda Serikali.

"...kazi iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha tunashinda uchaguzi wa rais na tunashinda viti vingi zaidi ili tuweze kuunda Serikali ijayo ya awamu ya tano itakayokuwa ya kwanza isiyo ya CCM. Mheshimiwa Lowassa kuanzia leo tutakapo kupa fomu hizi una haki ya kuzunguka Tanzania nzima na kuzungumza na Watanzania kuwaambia kuwa wewe ni mgombea uliyependekezwa na Chadema kugombea nafasi hiyo," alisema Lissu.

[caption id="attachment_60239" align="aligncenter" width="738"]Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza kabla ya Lowassa kukabidhiwa fomu za Chadema Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza kabla ya Lowassa kukabidhiwa fomu za Chadema[/caption]

[caption id="attachment_60248" align="aligncenter" width="800"]Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA. Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.[/caption]

[caption id="attachment_60249" align="aligncenter" width="800"]Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA. Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.[/caption]

[caption id="attachment_60248" align="aligncenter" width="800"]Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA. Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.[/caption]

[caption id="attachment_60246" align="aligncenter" width="800"]Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA. Wanachama wa Chadema waliofurika kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la Edward Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.[/caption]


[caption id="attachment_60240" align="aligncenter" width="800"]Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu (kulia) akizungumza jambo na Lowassa katika hafla ya kuchukua fomu ya kugombea kwa tiketi ya CHADEMA. Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu (kulia) akizungumza jambo na Lowassa katika hafla ya kuchukua fomu ya kugombea kwa tiketi ya CHADEMA.[/caption]

[caption id="attachment_60236" align="aligncenter" width="800"]Vijana wa ulinzi wa chadema wakisafisha njia kabla ya kuwasili kwa Edward Lowassa ofisi za Chadema Makao Makuu, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Vijana wa ulinzi wa chadema wakisafisha njia kabla ya kuwasili kwa Edward Lowassa ofisi za Chadema Makao Makuu, Kinondoni jijini Dar es Salaam.[/caption]

[caption id="attachment_60234" align="aligncenter" width="800"]Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwasili katika hafla ya kuchukua fomu ya kugombea kwa tiketi ya CHADEMA. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwasili katika hafla ya kuchukua fomu ya kugombea kwa tiketi ya CHADEMA.[/caption]

Baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumkabidhi fomu Lowassa walijitokeza baadhi ya wanachama na kumchangia fedha za kulipia fomu hiyo na kumkabidhi ili aongezee na kulipia fomu aliyochukua. Kwa upande wake Lowassa akizungumza mara baada ya kuchukua fomu aliwashukuru wanachadema kwa kumchangishia fedha za kulipia fomu na kudai hana cha kuwalipa lakini washirikiane aweze kushinda uchaguzi huo na matunda yake watayaona.

Alisema watu wanaoendelea kumshambulia mara baada ya kujiunga na Chadema wanapoteza muda bure kwani hawezi kurudi nyuma. Wale wachambuzi wa mambo wanaonishambulia baada ya kujiunga Chadema wanapoteza muda mimi sitarudi nyuma...mimi ningependa kuwaambia natekeleza maelekeza wa Baba wa taifa Mwalimu Julias Nyerere alisema 'Watanzania wanataka mabadiliko wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM, mimi nimeridhika ndani ya CCM mabadiliko hayo hayawezi kupatikana, lakini Watanzania wanataka mabadiliko mabadiliko haya watayapata kwa kura zetu...wanaotaka mabadiliko ni wengi tukijipanga vizuri tutashinda uchaguzi," alisema Lowassa.

Kwa upande wake Mbowe alisema Agosti 4, 2015 Chadema itakuwa na Mkutano Mkuu ambao kwa kushirikiana na vyama vinavyounda UKAWA watapitisha jina la mgombea Urais pamoja na mgombea mwenza na pia kupitisha ilani ya uchaguzi ambayo imeridhiwa na vyama vyote vinavyounda umoja wa UKAWA kabla ya kuanza mchakato wa kampeni.

Alisema bado wanakipindi kikumu cha majadiliano na maridhiano ya vyama vyote vinavyounda UKAWA hivyo kuwataka wananchi wawaombee ili waweze kupita salama katika kipindi hicho kigumu. Kuanzia Agosti 5 hadi 7, 2015 Kamati Kuu itapitisha wagombea wa Ubunge kwa utaratibu ambao pia utatumiwa na vyama vyote vinavyoshirikiana katika umoja wa UKAWA.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)