Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255 sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani
Mgombea kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo
Mgombea nafasi ya Ubunge,Nsajigwa Mwakatobe aliyepata kura 6 sawa asilimia 2.18% akiwashukuru wajumbe wa mkutano pamoja na wanachama wa chama hicho
PIPOOOOZ!Mgombea nafasi ya Ubunge viti maalum Grace Macha alipata kura 3 katika kinyang'anyiro hicho , akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kushirikiana nao
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akisaini fomu ya uchaguzi,pembeni ni Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini
Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini akitaja washindi katka kinyang'anyiro hicho
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mtoto wake aliyemkimbilia mara baada ya baba yake kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)