Pages

JOB NDUGAI AMPIGA MGOMBEA MWENZIE WAKATI WA KUJINADI

Mbunge wa Kongwa aliyemaliza muda wake ambaye pia ni naibu spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amempiga mgombea mwenzie kwa nafasi ya ubunge, Dk. Joseph Chilongani kwa madai ya kumpiga picha wakati anafanya fujo
Tukio hilo limetokea jana jioni wakati wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM wakiwa kwenye mkutano na wanachama wa CCM kwa ajili ya kujinadi kwenye kata ya Ugogoni iliyopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mdogo wa Dk. Chilongani, Michael Chilongani, Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya mmoja wa wagombea anayeitwa Simon Ngatunga kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kuahidi kuwa kama atakuwa mbunge atahakikisha kuwa anaziba mianya yote ya ubadhirifu kauli iliyomkera Job Ndugai.
Ilipofika zamu ya Ndugai kujinadi kwa wanachama wa CCM alimtuhumu Ngatunga kwa kusema uongo na kwamba hakuna ubadhirifu wa aina yoyote ndani ya Halmashauri hiyo.


Amesema Ndugai aliposhuka jukwaani alianza kumtafuta Ngatunga ili ampige kwa fimbo ambayo huwa anatembea nayo kwenye kampeni hizo.
Wakati akifanya fujo za kumpiga mgombea huyo, Dk. Chilongani alikuwa anampiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi ambapo Ndugai alipomwona alianza kumshambulia kwa fimbo katika maeneo ya tumboni na kichwani hali iliyomfanya mgombea huyo kupoteza fahamu papo hapo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa hana taarifa kuhusiana na tukio hilo ambapo Job Ndugai simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)