Waziri wa zamani Daniel Yona akiituliza familia yake mara baada ya hukumu kutolewa leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam. |
Waziri wa zamani Basi Mramba akiteta na mawakili wake baada ya kuhukumiwa leo mahakamani Kisutu. |
kwenda jela miaka mitatu kila mmoja kwa kukutwa na makosa 10 ya matumizi mabaya ya madaraka. Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Uchumi Grey Mngonja (kushoto) ameachiwa huru bada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake.
Pia Mahakama hiyo imewahukumu kulipa faini ya shilingi milioni 5 au kwenda jela miaka 2 zaidi baada ya kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya shilini bilioni 11.7.
Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya
ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na
kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya
dhahabu nchini ya M/S Alex Stewart.
Hukumu iliyowatia hatiani ni ya wajumbe wawili kati ya jopo la Mahakimu watatu, ambao ni Jaji Samu Rumanyika aliyeanza kusikiliza kesi hiyo kabla ya kuapishwa kuwa Jaji na Hakimu Mkazi Mkuu Saul Kinemela. Crdt Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)