Watu 23 wahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya basi la "Another G" na Lori iliyotokea Mufindi Iringa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Watu 23 wahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya basi la "Another G" na Lori iliyotokea Mufindi Iringa

Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita  kushoto  akiwa na wajumbe wa kamati ya  ulinzi na usalama wilaya hiyo ya  Mufindi  katika  kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi
Baadhi ya  ndugu  wakichukua mwili wa ndugu  yao baada ya  kuutambua
Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto)   akimfariji  mmoja kati ya  majeruhi wa ajali ya  basi la Another G na  lori  iliyoua 23 na kujeruhi 34 jana  ,wengine pichani ni wajumbe wa  kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya  Mufindi (picha na matukiodaimaBlog)

 Na MatukiodaimaBlog


MIILI yote  23  ya ajali  ya  basi  aina  Coster  mali ya kampuni ya  Another G lenye  namba  za  usajili  T 927 CEF aina ya  mitsubishi fuso iliyokuw3a ikifanya safari  zake  kati ya Iringa – Njombe ambalo  liligoganga na   uso kwa  uso na lori  lenye namba za usajili T 916AQM  likiwa na  Tela lenye namba za usajili T 965 BEH Scania  imetambuliwa na  ndugu  zao.


Kwa  mujibu  wa  mkuu  wa wilaya ya Mufindi ambae ni  mwenyekiti wa kamati  ya  ulinzi na usalama ya  wilaya  Bi Mboni Mhita kuwa  ndugu  wa  marehemu  hao  waliokufa katika ajali  waliweza  kutambua  miili ya  ndugu  zao jana na leo na   kuwa hadi  sasa hakuna mwili  ambao bado  kutambulia na  hivyo kuvishukuru  vyombo  vya habari kwa  kushiriki  kuhabarisha  juu ya ajali  hiyo  na wananchi  ambao  waliitikia na   kufika  kutambua miili   hiyo .


Akizungumza na  mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz  leo  mkuu  huyo  wa  wilaya Bi Mboni  alisema  kuwa  jitihada  kubwa zimeonyeshwa na  vyombo  vya habari  vya ndani ya mkoa  wa Iringa na nje ya  mkoa ikiwemo mitandao ya  kijamii  katika  kuhabarisha  umma na ndio  sababu ya utambuzi  wa miili  hiyo  kufanikiwa mapema baada ya habari kuenezwa vilivyo.


Pia 
mkuu  huyo wa wilaya   alipongeza  uongozi  wa JKT Mafinga   na  
uongozi  wa kitaifa  wa jeshi   hilo kwa  kujitolea  kusaidia mazishi  
ya  vijana wake  ambao walikuwa wakielekea JKT Mafinga kwa ajili ya  
kuripoti kwa kuanza mafunzo ya jeshi na   baadhi yao  kufa katika ajali 
hiyo  huku baadhi  wakijeruhiwa kwani alisema ni  vigumu kwa taasisi  
kujitolea  kusaidia mtu ambae hana mkataba  nae.


Aidha 
mkuu  huyo  wa  wilaya aliwaomba  wananchi wote  nchini ambao ndugu  
zao walipoteza maisha katika ajali ya basi la Majinja lililoua  watu  
zaidi ya 50 katika  eneo la Changalawe  mjini Mafinga  kufika kituo  
cha  polisi Mafinga kwa ajili ya kutambua  na kuchukua mizigo ya  ndugu 
zao  waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwa mali  zote za 
marehemu hao zimehifadhiwa salama.

Hata 
hivyo  mkuu  huyo  wa  wilaya ya  Mufindi Bi Mboni alivitaka  vyombo  
vya   usalama  barabarani katika  wilaya ya Mufindi  kuendelea na  
mkakati  wake wa  kuwabana madereva wanaovunja  sheria  za  barabarani 
na kuwachukulia hatu kali kama  njia ya  kupunguza ajali  hiyo.


Alisema 
askari  hao  pia  wanapaswa  kukagua ubora  wa  vyombo  vya usafiri  
vyote na  vile ambavyo havina  ubora  ni heri  kuvifungia  hadi  
vitakapoboreshwa  kuliko  kuruhusu vyombo  vya  usafiri  chakavu  
kufanya kazi  ya usafirishaji  wa abiria .


Kuhusiana 
na wajibu  wa  shirika la viwango Tanzania (TBS) mkuu  huyo wa wilaya   
alishauri kuwepo na mkakati makini wa TBS  kukagua  ubora  wa vyombo   
vya usafiri vinavyoingizwa  nchini kwani mabasi  mengi ya abiria  siti  
zake zimeshikiliwa na ngundi ya mbao na baada ya kutokea ajali siti 
hizo  hung'oka na kama abiria amefunga mkanda hulazimika kuchomoka na 
siti yake .


Alisema 
katika ripoti ya ajali ya kwanza ya basi la Majinja  iliyotokea Machi  
mwaka huu na kuua watu zaidi ya 50   kamati ya uchunguzi  ilibaini hilo  
na  kuwa  mwenye uwezo wa  kukagua  viwango  vya vyombo  hivyo  vya  
usafiri ni TBS kwa kushirikiana na wadau wengine kama Sumatra   na jeshi
la polisi  kupitia kitengo  cha usalama barabarani.


Wakati  
serikali ya  wilaya ya  Mufindi kupitia mkuu  huyo wa  wilaya ikishauri 
TBS na  washirika  wake  kuweka mkakati wa kukagua   viwango  vya  
vyombo   hivyo  vya usafiri baadhi ya  wananchi   wilaya ya  Mufindi na 
mkoa wa Iringa wamekuwa na maoni  tofauti kwa  kulitaka jeshi la polisi 
kitendo  cha askari wa usalama barabarani kuanza kusindikiza mabasi hayo
yanayotoka  usiku mkoani Njombe na Iringa ili  kuhakikisha abiria   
hawazidi katika mabasi hayo ya usiku.


Zacharia 
Sanga  mkazi  wa Mafinga  wilaya ya Mufindi na John Lumwesa mkazi  wa  
Iringa mjini  walisema kuwa  kimsingi mabasi hayo  yanajaza  abiria   
kupita  kiasi na kutembea kwa mwendo mkali  zaidi kutokana na nyakati za 
usiku  askari  wa usalama barabara  kutokuwepo.


Hivyo 
walitaka  askari  wa usalama barabarani  kuendelea kuwepo na tochi hadi 
usiku ili  kuthibiti ajali mbaya kama  hiyo ambayo mbali ya  kuwa ni 
uzembe wa dereva  wa basi ila kukosekana kwa askari  wa usalama  
barabarani  usiku ni  moja ya  sababu.


Mganga  mkuu  wa  
Hospitali  ya  wilaya ya  
Mufindi Dr  Godluck  Mlimbila  alisema  
kuwa hali za majeruhi 34 waliokuwa  wamelazwa katika  Hospitali   hiyo  
zinaendelea  vizuri na  kuwa mbali ya  wale  wanne ambao  hali  zao  
zilikuwa mbaya  zaidi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya   mkoa 
wa Iring
katika Hospitali  hiyo hadi jana majira ya saa 8 mchana  ni majeruhi  
kati ya 8 na 10  pekee  ndio ambao  walikuwa  wakiendelea na matibabu    
huku  wengi  wao wakiwa  wameruhusiwa baada ya hali  zao  kuendelea   
vema .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages