Pages

MKE WA MWANAHABARI WA KAMPUNI YA GUARDIAN NA NIPASHE, THOBIAS MWANAKATWE AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM JANA

 Mke wa Thobias Mwanakatwe, Levina Michael Genda,  enzi za uhai wake.
 Mwanahabari Thobias Mwanakatwe, aliyefiwa na mke wake.
Mwanahabari Thobias Mwanakatwe, akiwa na mke wake enzi za uhai wake.

Dotto Mwaibale

MWANAHABARI wa Kampuni ya The Guardian na Nipashe, Thobias Mwanakatwe, amepoteza mke wake baada ya kugongwa na gari eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana usiku majira ya saa 2;30.

Akizungumza na mtandao huu Mwanakatwe amesema kifo cha ghafla cha mke wake ni pigo kubwa kwake na familia zote mbili.

Mwanakatwe amesema shughuli za kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika kesho kuanzia saa tano na baada ya hapo watausafirisha kwenda kijiji cha Endala Karatu mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika kesho kutwa.

Kama kuna yeyote atakaye penda kumtolea chochote mwenzetu Mwanakatwe ili kimsaidie kwa msiba huo anaweza kuwasiliana naye kwa namba hizi za simu-0762-183666, 0655-183666 na 0787184666. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)