Misikiti minane kufungwa Tunisia
Utawala nchini Tunisia unasema kuwa utafunga misikiti 80 katika kipindi cha wiki moja inayokuja kwa madai ya kuhubiri chuki na jihad.
Hii ni kufuatia shambulizi lililofanyika kwenye hoteli moja hapo jana ambapo takriban watu 39 wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya ulaya waliuawa na mwanamme mmoja aliyejifanya kuwa mtalii.
Wapiganaji wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kundi la kiislamu la Islamic State wamesema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulizi hilo.
Waziri mkuu nchini Tunisia Hanib Essid anasema kuwa misikiti hiyo ndio iliokuwa ikitumika kueneza propaganda na kuunga mkono ugaidi.
Hali ya usalama umeimarishwa maradufu katika maeneo mengi mjini Tunis na karibu na majengo yenye watalii wengi.
Tayari wanajeshi wa akiba wameamrishwa kuripoti mara moja katika kambi za jeshi zilizoko karibu nao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)