MH.WAZIRI WA FEDHA SAADA M.SALUM AFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI WA MASHINE ZA EFD KATIKA MADUKA MKOANI DODOMA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MH.WAZIRI WA FEDHA SAADA M.SALUM AFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI WA MASHINE ZA EFD KATIKA MADUKA MKOANI DODOMA.

1
Mh.Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum(MB) akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA mkoani Dodoma (mwenye miwani) na wakala wa TRA kutoka Yono Action Mart kulifunga duka la Salome Furniture baada ya kukutwa akifanya biashara bila ya kutumia risiti za mashine ya EFD.2
Mh.Waziri wa Fedha Mhe. Saada M.Salum(MB) akimsikiliza msimamizi wa duka la Salome Furniture wakati akijitetea baada ya kukutwa anafanya biashara bila ya kutumia mashine ya EFD.3
Waziri wa Fedha Mh. Saada M.Salum(MB) akiwa katika mgahawa wa Dodoma Carnival alipotembelea kukagua matumizi ya mashine za EFD. Mh.Waziri aliagiza mgahawa huo ufungwe mpaka hapo watakaponunua mashine hizo. Kushoto kwa Mh.Waziri ni meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma na mwenye shati jekundu ni msimamizi wa mgahawa huo.4
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (MB) akiwa na Mh.Rukia Kassim Ahmed Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha wananchi CUF wakitoka kwenye duka ambalo lilikutwa mmiliki wake akifanya biashara bila ya kutoa risiti za mashine ya EFD. (Picha zote na Ramadhani Omary).5
Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (MB) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi.Ingiahedi Mduma mara baada ya kufanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD katika duka mojawapo Mkoani  Dodoma
.……………………………………….
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum amefanya ukaguzi wa ghafla katika baadhi ya maduka Mkoani Dodoma ili kuona kama maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD yanatekelezwa ipasavyo.
Katika ukaguzi huo ambao ulihusisha maduka ya kuuza thamani za majumbani,nguo na maduka ya kuuza bidhaa mchanganyiko (Mini supermarket).

Mh.Waziri akiongozana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliagiza kufungwa kwa maduka yote ambayo yamekaidi agizo la Serikali la matumizi ya mashine EFD mpaka pale watakaponunua na kuzitumia ipasavyo mashine hizo.

Aidha Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuisaidia Serikali kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na ambao wanapelekea kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetumika katika kuboresha huduma za kijamii.


Imetolewa na Msemaji Mkuu,

Wizara ya Fedha
Dodoma

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages