Pages

MBUNGE WA KIGAMBONI DK. FAUSTINE NDUGULILE JUMAMOSI KUFUNGUA MASHINDANO YA DIWANI CUP

 Diwani wa Kata ya Kisarawe Two, Issa Zahoro, mwanzilishi wa mashindano hayo.
 Diwani wa Kata ya Kisarawe Two, Issa Zahoro, akimkabidhi jezi na mpira Nahodha wa Timu ya Nyati, Saidi Momba kwa ajili ya mashindano hayo.
 Diwani wa Kata ya Kisarawe Two, Issa Zahoro (kulia), akimkabidhi vifaa vya michezo Mwakilishi wa Timu ya Soka ya Mwasonga, Saidi Simba Dar es Salaam leo asubuhi  kwa ajili ya michuano ya Diwani Cup katika kata hiyo yenye kauli mbiu 'Umoja ni Mshikamano" yatakayoanza Jumamosi Juni 20 mwaka huu.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Ayub Mkonde (katikati), akitoa nasaha zake kwa wanamichezo hao baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo. Kulia ni Mratibu wa Mashindano hayo, Stephen Nditi na Diwani wa Kata hiyo, Issa Zahoro.
 Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Sofrety Magesa akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Lingato, Cosmas Kalimanzila.
 Mratibu wa Mashindano hayo, Stephen Nditi (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.



 Jezi na mipira walivyokabidhiwa wanamichezo kwa ajili ya mashindano hayo.
 Wanamichezo kutoka Kata hiyo wakisubiri kukabidhiwa 
vifaa vya michezo.
Wanamichezo kutoka Kata hiyo wakisubiri kukabidhiwa 
vifaa vya michezo.

Dotto Mwaibale

MBUNGE   wa Jimbo la Kigamboni,  Faustine Ndugulile anatarajiwa kuwa mgeni rasimi katika mashindano ya Diwani Cup Kata ya Kisarawe Two iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar  es salaam.

Akizungumza Dar es Salaam leo na wandishi wa habari wakati wa kukabidhi  vifaa kwa timu 13 zitakazo shiriki mashindano  hayo diwani wa  kata  hiyo  Issa Zahoro alisema kuwa lengo la mashindano hayo nikuwazuia vijana kutojihusisha na utumiaji wa madawa yakulevyapamoja nakuibua vipaji vyao kisoka.

Alisema kuwa mashindano hayo yatatoa nafasi   kwa vijana hao kuonesha vipaji vyao na hatimaye kujijengea mazingira mazuri  yakuichezea timu ya taifa ya tanzania  taifa stars 

Alizitaja timu zitakazo shiriki michuano hiyo   itakayoanza kutimua vumbi june 20 mwaka huu katika viwanja  vya Arsenal pamoja na Kibomade vilivyopo katika kata hiyo kuwa ni Dubu, Tumaini, Simiyu, Home boys, Mwasonga, Mkamba, Mapinduzi, Sharifa,  Sire, madege, Kichangani, Diciprine naNyati.

Zahoro alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh.500,000 na mshindi wa pili 300,000 na wa tatu 200,000 na kuwa zawadi zingine zitatolewa kwa mchezaji bora, kipa bora, timu yenye nidhamu na mfungaji bora. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712727062)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)