Pages

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA RASMI MATANGAZO YA TELEVISHENI YA MFUMO WA ANALOJIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za Ukomo wa matangazo ya Televisheni ya Analojia, zilizofanyika leo Juni 17, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Meza Kuu
Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Tanzania, TCRA, Prof, John Nkoma, akizungumza juu ya kuhama kutoka katika mfumo wa analojia kwenda mfumo mpya wa digitali katika sherehe za kuhitimisha uhamaji wa mfumo wa analojia kwenda digitali iliyofanyika katika ukumbi wa mlimani city mapema leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma, wakati wa sherehe hizo.
Baadhi ya wawakilishi kutoka makampuni mbalimbali ya watoa huduma za warusha matangazo ya televisheni, wafanyakazi wa TCRA na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe hizo za kuhitimisha uhamaji wa mfumo wa analojia kwenda digitali iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Ngao ya Heshima za Digital Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Tanzania, TCRA, Prof, John Nkoma, wakati wa sherehe za Ukomo wa Matangazo ya Televisheni ya Analojia, zilizofanyika leo Juni 17, 2015 kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa. (wa pili kulia) ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo , Dkt. Fenella Mukangara
 Picha ya Pamoja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Ngao ya Heshima za Digital Tanzania, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof, Makame Mbarawa, wakati wa sherehe za Ukomo wa Matangazo ya Televisheni ya Analojia, zilizofanyika leo Juni 17, 2015 kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Wa pili (kulia) ni  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara. ( kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)