Pages

Filamu ya Mpango Mbaya kuzinduliwa leo Mlimani city, huku siti zikiwa zimeshajaa mpaka sasa

Filamu ya mpango mbaya imechezwa na washiriki wa shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki wa season One ndio wahusika katika Filamu hii.

Filamu hii imechezwa na washiriki wa shindano hilo huku wasanii wachache wakiwa wameshirikishwa Mpangilio wa maudhui katika filamu hii ni wa hali ya juu huku filamu hii ikiwa na ubora wa hali ya juu kuanzia ubora wa sauti, picha na kadhalika na kupelekea walioiona mwanzo kusema kuwa inaweza kuchukua tuzo hata hollywood kutokana na teknolojia iliyotumika.

Filamu hii inazinduliwa leo Mlimani city kuanzia saa 12 jioni huku siti zote zikiwa zimejaa mpaka sasa

Ubora wa kazi ya washiriki wa TMT 2014 na filamu hii inatarajia kuirudisha tasnia ya filamu nchini kupendwa na watu wa ndani ambao walipoteza matumaini kutokana na filamu nyingi kutokuwa na ubora wala stori zisizoeleweka huku nyingi zikiwa za mapenzi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)