Washiriki wakisubiri hukumu kutoka kwa majaji wa TMT 2015 #mpakakieleweke.
Mara baada ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT 2015) #mpakakieleweke kumalizika Kanda ya Ziwa na kupelekea kupatikana kwa washindi watatu kutoka kanda ya ziwa na Kupelekea shindano hilo kuhamia Kanda ya Kaskazini huku usaili wake ukiwa umeanza tarehe 2 May 2015, Shindano hilo limeingia hatua ya tatu na ya mwisho huku washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini wakipatikana.
Takribani washiriki wapatao 350 waliojitokeza kushiriki katika Shindano la Tanznaia Movie Talents (TMT) #mpakakieleweke waliweza kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao huku mchuano ukiwa mkali kwa vijana hao waliojitokeza huku wengi wakiwa na vipaji vya kweli. Shindano la Tanzania Movie Talents 2015 (2015) #mpakakieleweke limefikia tamati leo kwa kuwapata washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini ambao mara baada ya kupatikana walikabidhiwa zawadi zao za Shilingi laki Tano taslimu huku wakisubiria kwenda Dar es Salaam kwaajili ya kuiwakilisha kanda ya Kaskazini katika safari ya Kuwania Zawadi Kubwa kabisa ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania kwa Mshindi wa Kwanza. katika fainali itakayofanyika Mwezi wa nane Jijini Dar. Mara baada ya washindi kupatikana Kanda ya Kaskazini hatimaye filamu ya washirikiwaliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora katika shindano la TMT mwaka jana 2014 itazinduliwa mnamo tarehe 6 may 2015 katika ukumbi wa blue fame uliopo katika viwanja vya triple A Jijini Arusha
Mara baada ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT 2015) #mpakakieleweke kumalizika kanda ya Kaskazini shindano hilo litaendelea kufanyika kanda ya kati ambapo usaili utafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 May huku likitanguliwa na uzinduzi wa filamu ya washiriki wa TMT mwaka 2014.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke limepigwa tafu na I-view Studio, Global Publishers, Precision Air na ITV na Radio One
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)