Arusha, 29
Mei 2015. Nguli wa vifaa vya umeme
Samsung imeendelea na juhudi za kuimarika katika nafasi ya kwanza kwa uzinduzi
wa simu zake mpya na za kushangaza za 4G LTE zilizopewa jina la ‘Muvika’.
Uzinduzi huu wa mara ya kwanza na wa aina yake nchini kwa upande wa simu za
mkononi zenye teknolojia ya aina hii ulifanyika Hoteli ya Bay Leaf Arusha.
Pamoja na utambulisho huo tukio lilikuwa kama jukwaa la usimamizi wa
wazalishaji simu kukutana na wafanyabiashara wa hapa nyumbani, mawakala na
wadau wengine muhimu.
Soko la simu za mkononi Arusha ni moja kati ya yale
ambayo kampuni inayatazama kama fursa ya pekee na ilikuwa sababu ya kuchagua
Arusha kwa uzinduzi wa 4G LTE mbali na Dar es Salaam. Kutokana ukuaji wa uchumi
mkoani hapa na sekta kama za utalii na madini zinazosaidia katika maendeleo ya
kiuchumi makampuni mengi kama Samsung yanakuja kwa kasi kuhakikisha
huduma/bidhaa zao haziko mbali na wateja wao muhimu.
Uzinduzi ulifanyika
mbele ya wageni waalikwa kutoka mkoani hapo kukiwa na burudani ya moja kwa moja
kutoka kwa ‘msanii maarufu’ na balozi wa kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung
Tanzania Vanessa Mdee.
Akiongea wakati wa sherehe za uzinduzi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya vifaa vya
umeme ya Samsung Tanzania Bw Hyeongjun Seo, aliongelea mahusiano mazuri
yaliyopo kati ya kampuni na watu wa Arusha na umuhimu wa kuzingatia huduma bora
na bidhaa inayoendana na Samsung. Alisema “Arusha
ni mkoa muhimu kibiashara na hatuangalii tu kuendelea kutoa ubora wa uzoefu
wetu kwa wateja lakini pia kuwapa bidhaa za kisasa na za kibunifu zinazoendana
na soko la kimataifa.”
Maoni ya Mkurugenzi mtendaji yaliungwa mkono na Sylvester Manyara, Mkuu wa Mauzo na
Usambazaji Samsung Electronics Tanzania akisema “Leo tunazindua teknolojia hii katika uwepo wa mawakala na wasambazaji
wetu, tumechagua Arusha ikiwakilisha nia ya kuendelea kukua ambako ni sehemu ya
utamaduni wa Samsung.”
‘Muvika’ ni neno lisilo rasmi linalojaribu kuelezea
uwezo wa simu hii na wepesi wake katika mtandao unaokuja na 4G LTE
unaowawezesha watumiaji kupata hadi filamu kwa kasi ya kushangaza. 4G LTE
(Mabadiliko ya Kudumu ya Kizazi cha Nne) ni simu yenye teknolojia ya kisasa
katika mtandao inayoipeleka Dunia kwa kasi. Kwa mahitaji yanayoongezeka ya simu
za kisasa zenye uwezo kama huu Samsung Tanzania wanahakikisha kuwa mahitaji ya
wateja wao yanafikiwa.
Akiwa kama balozi wa bidhaa za Samsung Tanzania Bi
Vanessa Mdee atakuwa kama uso wa simu zitakazotolewa chini ya mwamvuli wa Muvika.
Akichangia juu ya wajibu wake Vanessa alisema “Huu ni ukurasa mwingine mzuri zaidi tunaoufungua na Samsung tangu
tulipoianza safari yetu pamoja na kama mzaliwa wa Arusha nafurahi kupata fursa
hii kuwa mstari wa mbele wa mabadiliko ya teknolojia ambayo Samsung
wanaanzisha”
Mwisho
Kuhusu
Vifaa vya kielektroniki vya Samsung
Teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu takribani
236,000 katika nchi 79, inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia kuingia kwenye
teknolojia mpya na matumizi ya smart phone, luninga, air-conditioner, vifaa vya
nyumbani vya kieletroniki, kamera, na vifaa vya maofisini kama kompyuta na
printers ambavyo vina teknolojia ya hali ya juu kukidhi mahitaji ya wateja.
Kujifunza mengi zaidi, tembelea www.samsung.com na www.facebook.com/SamsungMobileTanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)