Kwa
kuwa magonjwa ya mishipa ya moyo ayajitokezi ghafla, inaweza kuchelewa
kugundulika mpaka mtu anapopata mshtuko wa moyo. Ingawa kulingana na madaktari
bado watu wengi wanaweza kujizuia na pia kutibiwa magonjwa ya mishipa ya moyo
na wanashauri waanze kwa kubadili mtindo wa maisha kiafya.
Matibabu
ya mishipa ya moyo (CAD) yanategemea ni kiasi gani ugonjwa umekuwa. Kubadili
mtindo wa maisha ni hatua za kwanza zinazoshauriwa kwa yeyote mwenye ‘CAD’.
Kiafya tabia huweza kupunguza au kusimamisha kasi ya ugonjwa na kuimarisha
ubora na urefu wa maisha ya mgonjwa. Tabia hizi ni pamoja na; kuacha kuvuta
sigara na kujikinga moshi wa sigara ya mvutaji mwingine, kula chakula bora,
mazoezi ya mara kwa mara, kudhibiti uzito, kutuza afya ya ubongo na kudhibiti
hali kama shinikizo la damu, kolesteroli na kisukari.
Kwa
watu ambao ugonjwa huu umeshakuwa ndani yao, maendeleo yameleta mapinduzi
katika matibabu ya magonjwa ya mishipa ya moyo. Kati ya waanzilishi ni Dkt. Sathyaki Nambala, mshauri mwandamizi
na Mkuu wa kitengo cha upasuaji moyo, Hospitali ya Apollo; Bangalore. Dkt.
Nambala anafahahamika kama moja ya watu wanaoongoza nchini India kwa
upasuaji wa moyo, mapafu na mishipa. Anachukuliwa kama muanzilishi wa upasuaji
moyo wenye madhara madogo, hatua ambayo ni bora zaidi katika matibabu ya
magojwa ya mishipa ya moyo. Ni mbinu mpya na ya kisasa zaidi ya kuilinda
mishipa ya moyo na magonjwa. Kama jina linavyojieleza ni vitu vichache sana
vinavyotumika katika upasuaji wa moyo, katika mbinu hii moyo unafikiwa kupitia
upande wa kushoto wa kifua kwa kuingia ndani kwa sentimita 4. Upasuaji unafanyika
chini kidogo ya chuchu. Kifua kinapasuliwa katika mbavu pasipo kukata mfupa
wowote na kwa kutenganisha nyama. Kama ilivyo kwa upasuaji wa kawaida wa moyo
upasuaji huu unafanyika kwa kutumia mishipa yote au mchanganyiko wa mishipa na
mishipa inayotolewa kwenye mguu. Mishipa kutoka kwenye miguu katika upasuaji
huu pia huondolewa ndani kwa ndani bila kukata ngozi ya mguu. Vifaa vya kisasa
zaidi na mbinu za kisasa vinaruhusu upasuaji kufanyika kwa usalama zaidi.
Kulingana
na Dkt. Nyambala upasuaji wa mishipa
ya moyo wenye madhara madogo una faida kadhaa kuliko mbinu za kawaida. Kwanza
kabisa ni kuwa hakuna mfupa unaokatwa. Hii ina faida kadhaa katika kupunguza
maumivu, mwili kufanya kazi kama kawaida, na kupumua vizuri. Tofauti na
upasuaji wa kawaida wa moyo ni spidi ya kurudi kwenye maisha ya kila siku ikiwa
ni pamoja na kuendesha au shughuli nyingine ndogo ndogo ambazo mtu anaweza
kuendelea mara baada tu ya upasuaji.
Pili,
upotevu wa damu ni mdogo na pengine usiwepo kabisa jambu linalo ondoa mtu kuongezewa
damu na kuepusha maambukizi katika damu na mifupa. Tatu maambukizi yote
yanapunguzwa, iwe maambukizi katika kidonda au maambukizi katika mapafu baada ya
upasuaji. Hii inafanya mbinu hii kuwa muhimu kwa wagonjwa wenye kisukari na
wazee ambao wana kinga dhaifu kuzuia maambukizi
Nne,
upasuaji huu ni wa kistaarabu na kwa kipimo cha inchi 2 hadi 3 tu kiuhalisia ni
ngumu kuona kuwa upasuaji wa moyo umefanyika. Madaktari wakiwemo wale wa moyo
wanaelezea inavyoshangaza kwa jinsi ambavyo upasuaji wa moyo umefanyika kupitia
uwazi mdogo hivi.
“Katika upasuaji wa mishipa ya moyo wenye
madhara madogo (Minimal Invasive Cardiac Surgery) hakuna kuchimba au kukata
mfupa katika kifua. Mbinu ya kupitia kifua cha kushoto inaruhusu kupona haraka
bila usumbufu wa kidonda”. Anasema Dkt. Nyambala anaelezea zaidi kuwa “Hatua hii ni muhimu kwa wagonjwa wa kisukari na wazee. Kiwango cha
maambukizi kinakaribia sifuri na maambukizi katika mifupa yanazuilika kabisa.
Mishipa yote ya moyo na kuta zake huweza kutibiwa kwa usalama, kuifanya
upasuaji huu uliyo kamili usiolinganishwa na mbinu yoyote ya zamani.
Manufaa
haya yote kwa pamoja yanafanya mgonjwa kuchukua muda mfupi hospitalini na
kupona. Kizuri zaidi ni kuwa tofauti na mbinu za zamani, kuta zote bila kujali
zilipo katika moyo huweza kupitiwa katika hali salama na ya kueleweka.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)