Pages

Swali letu la Msingi leo:Unachukualiaje kauli hii ya kondata soma hapa

Abiria wakiwa ndani ya Daladala.Picha na Josephat Lukaza

Hivi kwa wale ambao hutumia usafiri wa daladala kutoka nyumbani kwenda mahala popote pale ndani ya jiji la Dar lazima utakuwa ushakutana na maneno ambayo makonda wanayatumia kila iitwayo leo kutokana na abiria kuwa wengi maneno ni mengi ambayo makonda huyatumia lakini leo tuangalie hili la Kuwaambia Abiria "Sogea nyuma wewe na wenzio wapande" au "rudi nyuma bwana mtu mzima hapangwi" na mengi ya namna hiyo na maneno haya mara nyingi makonda hutumia pindi ambapo abiria wanapanda na huku basi likiwa limejaa na kutaka kuendelea kupakia zaidi na mbaya zaidi wasione kaupenyo kidogo kwa juu utasikia tu hayo maneno bila kukumbuka kuwa chini hakuna sehemu ya kukanyaga...

Swali letu la msingi leo ni kwamba unajisikiaje au unachukuliaje kauli hiyo pindi konda anapokwambia hayo maneno ilihali hakuna sehemu ya kusogea?Unamchukuliaje na yeye?

Tupe maoni yako kupitia josephat.lukaza@gmail.com au toa maoni yako hapo chini sehemu ya kuchangia hapo chini

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)