Pages

Mama wa Mitindo Asia Idarous Khamisin afiwa na Mama yake mkubwa Zanzibar

IMG_3895
Na Mwandishi Wetu
MBUNIFU mkongwe wa mavazi, Mama wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin amepata pigo kufuatia kufiwa na Mama yake mkubwa, Aliyefahamika kwa jina la Fatma Juma, Msiba uliotokea Kisiwa Ndui, Unguja.

Kwa mujibu wa taarifa za msiba huo ambao hata hivyo tayari mazishi yake yamefanyika siku ya Jumatatu ya Mei 25, Kisiwa Ndui, na leo Jumatano ya Mei 27 wanatarajia kufanya kisomo maalum.

Ratiba ya Kisomo:
Leo Jumatano ya Mei 27, saa 10, Alasiri wanatarajia kufanya kisomo maalum kwa wanawake wote nyumbani kwa marehemu, Kisiwa Ndui na kwa upande wa Wanaume wao wanatarajia kufanya kisomo, majira ya saa mbili usiku.

Tunampa pole Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kufiwa na Mama yake mkubwa na mlezi. "Inna lillahi wa inna ilayhi rajiiun, mwenyezi mungu amlaze pema peponi".

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)