Pages

Ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio yajadiliwa na Kamishna wa fedha za nje

 Kamishna wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio  katika nchi za Africa.
 Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Kanda ya Afrika  wakimsikiliza na kufuatilia kwa makini Dkt. Mulu Ketsela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Benki hiyo.
 Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha   na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha kuhusu serikali ya Tanzania ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika kutekeleza mipango yake hasa  kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete  na kushoto kwake ni  Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard.
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha   na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka  nchini Rwanda, Ethiophia, Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)