Pages

Bayport: Wa mikoani nao wanaweza kukopa viwanja vya Kibaha

Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha, Obed Katonge, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliyofanyika mwishoni mwa wiki, katika hoteli ya Serena.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TAASISI ya Kifedha ya Bayaport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo,imesema hata Watanzania wanaoishi mikoani wanaweza kutumia fursa ya kukopeshwa viwanja katika mradi wa Vikuruti, uliopo Kibaha, mkoani Pwani. Unaweza kuptata fomu hapa.

Bonyeza hapa kupata fomu ya mkopo wa viwanja kutoka Bayport Financial Services

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua huduma ya mikopo ya viwanja katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyyo atoke Dar es Salaam au
Kibaha.
Kicheko cha furaha. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akifurahia jambo na Meneja Masoko na Mawasiliaano wa Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam.

Habari; Watanzania wengi wanaoishi mikoani wamekuwa wakiulizia kama nao wana weza kukopeshwa viwanja hivyo,hivyo Bayport imeona itowe ufafanuzi huu. Kwamba ni ruhusa. Kilaa mtu anaweza kukopa.

Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio maana wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali, bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.

“Nafasi ni chache, maana maombi yetu yanafanyika kwa siku (20), kuanzia ile Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services, bila kusahau kupitia bank of Africa (BOA), ambapo malilipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.

“Fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi yetu ya Bayport zilizoenea nchi nzima, huku baada ya Juni 10, mteja akitakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka Bayport, ambapo watumishi wa umma na wa kampuni wanaweza kukopeshwa kiwanja na wakikabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90), baada ya kukamilisha mkopo wake kwa wateja wa fedha taslimu na wengineo wakipewa baada ya kumaliza mkopo wao,” alisema Cheyo.


Kwa mujibu wa Cheyo, huduma ya mikopo ya viwanja ni maalum kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania wote waliokuwa wakitatizwa na suala zima la makazi, hususan kutokana na ugumu wa maisha unaowakumba Watanzania wengi nchini.


Ngula alisema kukaa mikoani si sababu ya kushindwa kukopa kiwanja kwa sababu wamefungua matawi katika wilaya na mikoa mbalimbali, hivyo ni jukumu la  mjasiriamali, mtumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi wanatumia nafasi hiyo kujiendeleza kwa kupata viwanja hivyo.


Naye Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit
Mndeme, aliliambia gazeti hili kuwa ukubwa wa viwanja hivyo unaanzia hatua 15 kwa 16, huku thamani yake ikianzia Sh 1,400,000 bila riba (mortgage), ambapo  pia fomu zao zimejieleza na kujifafanua vizuri kwa ajili ya kutoa urahisi wa kuwahudumia Watanzania wote.


Mndeme alimaliza kwa kuwataka wateja wao na Watanzania kwa
ujumla kujitokeza kwa wingi kuchangamkia viwanja hivyo vinavyokadiliwa kuwa 1878 vilivyokuwa katika eneo zuri, kilomita 50 kutoka Kisutu, jijini Dar es Salaam na kilomita 6.5 kutoka barabara Kuu ya Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)