Kamishna wa Fedha
za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano yanayohusu ya ripoti ya
utekelezaji wa mpango wa mafanikio katika nchi za Africa.
Wajumbe
waliohudhuria Mkutano wa Kanda ya Afrika
wakimsikiliza na kufuatilia kwa makini Dkt. Mulu Ketsela ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Benki
hiyo.
Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa
ufafanua wa masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile ambaye
amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Ethiophia Mhe.
Fisseha Aberra.
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha
kuhusu serikali ya Tanzania ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika
kutekeleza mipango yake hasa kwenye
miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete na kushoto kwake ni Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania
inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchini Rwanda, Ethiophia, Kenya na Visiwa vya
Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo
kila nchi imejiwekea.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)