Ni furaha yangu kubwa
kuwaalika leo hii kwenye uzinduzi wa NEMBO mpya ya kampuni ya ALAF.
Nichukukue nafasi
hii kuwaeleza kwa kifupi kuhusu ALAF
Kamuni ya ALAF, ilikuwa
ikijulikana kama ‘Aluminium Africa Limited’, ilimetimiza miaka 50 mwaka 2011.
Mwaka 1960, ALAF ilianza shughuli zake mjini Dar-es-Salaam. Kwa siku zile,
ilikuwa ni kampuni ya kwanza Afrika Mashariki kuweka kiwanda cha kuzalisha
chuma cha kukunjwa (kwa ajili ya masufuria), Mabati na Vyuma vigumu vya
kuezekea
ALAF ilitaifishwa
mwaka 1973 na kubinafsishwa mwaka 1997 na imekuwa moja kati ya stori za
mafanikio katika Sera ya Serikali ya ubinafsishaji wa viwanda.
Leo hii ALAF tuna
mashine za kisasa zijulikanazo kama Cold
Rolling Mill Complex zenye uwezo wa kuzalisha bidhaa kama CRC na CRCA maarufu
kama ‘Metal Coating Line’ ambazo hutumika kuzalisha vyuma vya aluminium na Zinc,
Mabati ya kuezekea na pia tuna mashine nyingine ijulikanayo kama Tube Mills kwa
ajili ya kutengenezea mabomba ya chuma, na bidhaa nyingine mbalimbali. Teknolojia
yetu ya ‘Metal Coating Line’ ni ya aina yake Afrika nzima na ilichukuliwa
kutoka BIEC, Marekani.
ALAF inatoa bidhaa
za kuezekea kwa ajili ya majengo ya aina zote, Mabomba ya chuma, vifaa vya aina
zote vyenye nafasi kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika sekta ya ujenzi.
Bidhaa za ALAF zinaaminika zaidi na ni bidhaa zinazouzika zaidi Tanzania na
nchi za jirani.
Kwa bidhaa za
viwandani za kudumu, ALAF inatoa SAFLOK 700, bidhaa inayosaidia kuunganishia
mabati ya kuezekea mpaka mita 150 kwa urefu wakati wa kuezeka bila kutumia
misumari au bolti. Baadhi ya majengo yaliyotumia bidhaa hiyo ni jengo la
Mlimani City lililopo mjini Dar es Salaam, jengo la AICC Arusha, jengo la Ofisi
ya waziri mkuu Dodoma na majengo mengine mengi.
Bidhaa za ALAF
zinauzwa kwenye mataifa yote ya jirani kama Zambia, Malawi, Burundi, Rwanda,
Uganda n.k. hivyo basi kuingiza fedha za kigeni nchini.
Kwa miaka mingi ALAF
imeendelea kugundua njia mpya na namna ya kuhudumia wateja wake vizuri kwa
kutoa huduma na bidhaa zenye viwango vya kimatifa . Moja ya hatua
zilizochukuliwa na ALAF ni kuwafikia wateja wake kwa Karibu zaidi. Kuhudumia
wateja wake kwa ufanisi zaidi ALAF ilifungua kituo cha huduma mjini Arusha
2009, Mwanza 2012 na Mbeya 2013 kwa wateja wa mkoa wa Kilimanjaro, Kanda ya
ziwa na Nyanda za juu kusini Vilevile. Kwa kuongezea, ALAF walifungua
‘Showroom’ mbili (Roof Gallery) Dar es Salaam na Arusha. Vituo vya huduma za
ALAF na ‘Showroom’ zinasimamiwa na wafanyakazi wenye uzoefu na waliopewa
Mafunzo ya kutosha, wanaowashauri wateja kuhusu suluhisho bora la kuezekea.
Mwaka huu ALAF imepanga kifungua kituo kingine cha huduma Dodoma.
ALAF ni ya kwanza na
kampuni pekee ya aina yake nchini Tanzania kupewa ISO 9001:2000 na ISO
14001:2005 kwa kuzingatia viwango vya ubora wa bidhaa zake na kujitoa kwake
katika kulinda mazingira.
ALAF imekuwa
ikishinda Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora wa Mwaka (kwa kundi la viwanda vikubwa) Inayoratibiwa na shirikisho la
viwanda Tanzania (CTI). Kwa miaka nane ya mafanikio.
Kujitoa kwa ALAF ni
zaidi ya ubora wa bidhaa zake. Kama sehemu ya kujitoa kwake kwa mazingira, ALAF
imeanzisha mfumo ujulikanao kama ‘Light Weight Steel Truss System’ kuchukua
nafasi ya matumizi ya mbao kutengeneza kenchi za kuezekea. Bidhaa hii inaokoa
miti mingi, hivyo kuifanya bidhaa rafiki zaidi kwa mazingira.
Mabibi na Mabwana
ALAF inaendeleza
jitihada za kurejesha inachokipata kwa jamii na kutimiza wajibu wake kwa jamii zaidi
ya maneno. Kwa kushirikia na shirika la fedha (IFC), USA, , ALAF imezindua mpango wa elimu ya afya kwa ajili ya kuzuia na kutibu
Malaria, VVU/UKIMWI na kifua kikuu si tu kwa wafanyakazi wake lakini pia kwa
jamii inayozunguka viwanda vyake. ALAF ina zahanati ya kisasa yenye vifaa
kamili na mazingira bora kutoa tiba bure
kwa wafanyakazi wake na familia zao. Zahanati hii inasimamiwa na madaktari,
manesi na wafanyakazi wa Hindu Mandal Hospital.
Kama mwanachama
muwajibikaji kwa Jamii ya raia wa Kitanzania, ALAF imetanua msaada wake kwa
Mpango wa Chakula Duniani kwa watoto na kutoa mchango mkubwa kwa njia ya vifaa
vya kuezekea moja kwa moja kwa miradi ya shughuli za kijamii.
Mabibi na Mabwana
NEMBO mpya ya ALAF
inahusisha kiini cha kufikia ngazi mpya ya ubora ambao unaiweka ALAF nchini Tanzania
na nchi jirani kama watengenezaji wakubwa na wakuaminiwa zaidi wa mabati ya
kuezekea, mabomba ya chuma na bidhaa nyingine mbalimbali za ujenzi kwa viwango
vya kimataifa.
Utambulisho wa NEMBO mpya
ni pamoja muonekano mpya wa ALAF na ushirikiano wake na SAFAL Group ambayo ipo
katika nchi 11 kuanzia Ethiopia hadi Afrika Kusini katika maeneo 33.
Kwa hili ALAF inaanza
safari mpya pamoja na muonekano mpya ulioboreshwa. Jina, Lengo na maadili ya kampuni yetu havitabadilishwa.
Tunaposonga mbele,
ni muhimu kutazama nyuma kule tulipotoka na jinsi tulivyoendelea. Muonekano wetu
mpya unatupa fursa kubwa ya kuwa na nguvu mpya.
Tunaamini kuwa
washiriki wetu kibiashara watayapokea mabadiliko haya mazuri na kuendelea kutoa
ushirikiano wao kwa mafanikio ya baadae.
Mabibi na Mabwana
Asanteni tena kwa kuchukua
muda wenu katika ratiba zenu zenye majukumu mengi na kutoa ushirikiano kwa ALAF
katika tukio hili muhimu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)