Kama watoa huduma za afya wanaoongoza barani
Asia Hospitali za Apollo zimekuwa maarufu na kukubalika kwa mafanikio yake
kitabibu na kujitoa kwake katika kuboresha maisha ya watu. Katika hali ambayo hutokea
mara chache kati ya wataalamu wa utabibu Apollo waliendesha zoezi la
upandikizaji wa viungo kwa kipindi cha siku moja. Matukio yaliyofanyika tarehe
4 Mei 2015 chini ya Hospital kuu ya Apollo Chennai, India ilishuhudia timu ya
madaktari ikivuna viungo 23 tofauti tofauti vya mwili kutoka kwa watoaji
tofauti watano.
Utofauti wa tukio hili pengine ni kuwa ni mara
ya kwanza familia tano zilizofiwa kujitokeza kwa wakati mmoja na kukubali
kujitolea viungo vya mwili wa mpendwa wao marehemu aliyefariki punde ili kuokoa
maisha ya wengine. Kitendo hiki cha kihistoria kinaonesha Ubinadamu wa familia
hizi zilizo katika kipindi kigumu kimeushangaza ulimwengu wa kitabibu na katika
mchakato huu kuweka rekodi ya kiasi kikubwa cha viungo kuwahi kuvunwa kwa siku
moja.
Timu ya madaktari
100 wenye taaluma mbalimbali ilitumia sehemu 7 za vyumba vya upasuaji kwa
wakati mmoja kuvuna viungo 23 na kufanya upandikizaji wa viungo 10 kwa wakati
huohuo. Madaktari na wafanyakazi wasaidizi walifanya kazi masaa 12 kusaidia
tukio hili la kukumbukwa, iliyo ongeza tena sifa nyingine kwa mafanikio ya
Hospitali za Apollo katika kuendesha shughuli nyingi zaidi za upandikizaji
viungo duniani.
Katika kupongeza
ukarimu wa familia zilizojitolea, hospitali za Apollo ziliandaa sherehe kwa
lengo la kuelezea shukrani zao kwa familia hizi. Sherehe ilihudhuriwa na
muanzilishi na mwenyekiti wa hospitali za Apollo Dkt. Reddy, Makamo mwenyekiti,
Bi. Preetha Reddy na timu yote ya madaktari ambao walihusika katika kuhakikisha
mafanikio ya mchakato huu.
Akihutubia mkutano
Dkt. Reddy alisema “Leo, familia hizi zenye nia njema zimesaidia kuwapa nafasi
nyingine ya kuishi watu walio katika hatua za mwisho kwa viungo vyao kushindwa
kufanya kazi – na kitendo kitawahamasisha watu wengi zaidi kuchangia viungo.
Inahitaji dhamira ya ziada kiubinaadamu na kupevuka kwa dhamira ya uwajibikaji
wa familia kuzisaidia jamii, hospitali na madaktari kutoa nafasi mpya ya maisha
kwa wale wanaohitaji. Uhai wa binadamu haununuliki, na maisha ya mtu yanapoweza
kutoa uhai na matumaini kwa wengine wengi wanaohitaji, kwa hakika hakuna cha
kulipia!”
Watanzania wengi
katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakitafuta huduma za kitabibu zaidi
nchini India sababu ya maendeleo na urahisi wa huduma hizi nchini India. Kwa
sasa Tanzania zoezi la kujitolea viungo halupo, kuundwa kwa sera na taratibu za
mchakato huu katika nchi kutasaidia watu wengi. Nchi kama India wanafaidika kwa
kuwepo kwa sera hii inayoruhusu watu kufaidika kwa ukarimu wa wanafamilia wa
marehemu kujitolea viungo vya mpendwa wao au marehemu mwenyewe kujitolea.
Hospitali za Apollo zinaongoza
duniani kufanya shughuli nyingi na kufanikisha upandikizaji wa viungo duniani
na kuwa na matokeo mazuri zaidi kuliko duniani. Ni kitovu kikuu cha rufaa kwa
upasuaji usiokuwa na madhara makubwa na kinapokea Idadi kubwa ya wagonjwa
kutoka Dunia nzima ikiwemo Tanzania wakitafuta huduma bora na rahisi za
matibabu kwa kutumia muda mfupi pasipo kusubirishwa. Zaidi ya wagonjwa wakigeni
200,000 kutoka zaidi ya nchi 120 wamefanikiwa kutibiwa magonjwa mbalimbali
kitaalamu katika hospitali za Apollo.
Hospitali za Apollo hivi karibuni
zilipata Tuzo ya dhahabu ‘Golden Peacock’ kutoka
taasisi ya wakurugenzi, kwa kushirikiana na kitengo cha sera na uendeshaji,
Serikali ya India. Hii ni tuzo ya juu zaidi ya ubora wa biashara katika sekta
ya afya, na kuchukuliwa kama kipimo cha kiwango katika tuzo za ubora wa
kampuni. Hospitali za Apollo ilipokea tuzo hii kwenye sherehe iliyofana
iliyofanyika katika Mkutato wa 25 wa Dunia juu ya ‘Uongozi wa Ubora wa biashara
na Ubunifu’ hivi karibuni Dubai.
Kama tu ukarimu uliooneshwa na familia hizi 5,
kwa kujitolea viungo vya wapendwa wao, utakuwa tochi kuwaangazia wengine
kufwata mfano huu, inamaana kuwa wagonjwa wengi zaidi ambao viungo vyao viko
katika hatua za mwisho kushindwa kufanya kazi na wanaohitaji zaidi watafaidika
kwa mwanzo mpya wa maisha.
JINSI GANI VIUNGO HIVI VILIFAIDISHA WATU TOFAUTI:
Kutoka kwa marehemu watano waliojitolea, figo 10, pea 3 za
macho (jumla ya macho 6), mioyo miwili (2) na maini mitano (5) vilipatikana:
·
Maini mitano (5) yalitumika Apollo
·
Moyo mmoja (1) ulitumika Apollo na mmoja (1) Fortis
·
Figo nne (4) Apollo
·
Figo nne (4) zilitumwa KGH, Coimbatore
·
Figo moja (1) ilitumwa Hospitali ya Kamakshi
·
Figo moja (1) ilitumwa Hospitali ya Global
·
Macho sita (6) yalitumwa Sankara Nethralaya
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)