Lil Wayne na Christina Milian
Mwanamuziki wa mtindo wa RnB Christina Milan amethibitisha uvumi wa siku nyingi kwamba ana uhusiano na msanii wa muziki wa Rap LilWayne ambaye pia anamwakilisha katika kampuni yake ya Young Money Entertainment.
Wawili hao walionekana pamoja katika pigano la karne kati ya Bingwa Floyd Mayweather na Manny Paquiao mjini Las Vegas.
Katika mahojiano na mtandao wa Etonline, Milian alisema kuwa Wayne ni mtu muhimu sana kwake.
''Ni mtu muhimu sana kwangu,ninaishi naye huru na sote tunafurahia'',.alisema.''Hakuna kitu kizuri kama kuwa na hisia na mtu hatua ambayo inakufanya kutojali kitu ambacho watu wengine wanasema,ni hisia ambazo watu uhisi kwa kweli'',.
Na alipoulizwa kuhusu kuolewa na Lil Wayne alisema:''huwezi kujua,ninamaanisha kwamba penzi huchochea vitu vizuri kama hivyo'', alisema Milian aliyejawa na tabasamu.BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)