Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko
ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama.
Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
Daktari
Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato wakifurahia Pads za
Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi
Duniani.
****
Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero,
Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia.
Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi huahirisha shughuli za kimasomo kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao
Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi.
Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na hua wanadhani mwanamke peke yake ndo anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna
Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya Bajavero walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)