Pages

TaSUBa yatangazia umma nafasi za kozi kwa mwaka wa masomo 2015 /2016

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
(TaSUBa)
timthumb
TANGAZO LA KUJIUNGA NA CHUO
TaSUBa inawatangazia umma nafasi za kujiunga na kozi kwa ngazi ya Cheti (Certificate) na
Stashahada (Diploma) kwa mwaka wa masomo 2015 /2016
Kozi hizo ni kama ifuatavyo:-

  1. Sanaa za Maonyesho (Performing Arts):-
Muziki, Ngoma, Tamthiliya/Maigizo, Sarakasi na Sanaa za Ufundi

  1. Ubunifu na Uzalishaji wa Muziki (Music Design and Production)
  2. Picha Jongefu (Media Design and Film Production)
- Masomo ya sayansi ya Jamii, ICT, Kiswahili na Kiingereza yatafundishwa kwa wote.
- Mwombaji kozi namba mbili (2) na namba tatu (3) awe na ujuzi wa compyuta.
unnamed (3)Pichani miongoni mwa walimu wa TaSUBa wakionyesha igozo la ubunifu jukwaani chuoni hapo.
NGAZI YA CHETI KWA MIAKA MIWILI
Sifa za Kujiunga
- Aliyemaliza Darasa la Saba (Standard Seven) na ambaye hakuhitimu kidato cha Nne
- Aliyehitimu kidato cha Nne na hakufanikiwa kupata wastani wa “D” nne (4)
ANGALIZO:
- Ngazi hii ni kwa Masomo ya Sanaa za Maonyesho TU.
- Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM B
IMG_0404.jpg wanafunziBaadhi ya wanafunzi wa wakiwa katika moja ya shughuli za ngoma katika jukwaa chuoni hapo.
NGAZI YA CHETI KWA MWAKA MMOJA
Sifa za Kujiunga
- Aliyemaliza kidato cha nne na kupata wastani wa “D” nne (4)
ANGALIZO:
- Watakaofaulu wastani wa ‘B’ baada ya kuhitimu ngazi ya cheti wataruhusiwa kujiunga
na Stashahada (Diploma) kwa miaka miwili.
- Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A
a78f38f1d4L
Wanafunzi wa TaSUBa wakiwa darasani chuoni hapo.
NGAZI YA STASHAHADA (DIPLOMA)
Sifa za Kujiunga
- Awe amefaulu kidato cha sita na kupata principal pass 1 na subsidiary 1
- Awe amehitimu ngazi ya cheti cha sanaa za maonyesho na ufundi kwenye chuo kinachotambuliwa na NACTE
ANGALIZO:
- Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A
IMG-20130928-WA0000Miongoni mwa wasanii Mahiri hapa Nchini Tanzania, Baba Haji akiwa katika pozi wakati wa kuhitimu masomo yake. Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii waliopitia chuo hicho.
MAELEZO MENGINE
- FOMU za kujiunga zinapatikana Chuoni pia kwenye tovuti ya chuo www.tasuba.ac.tz
- Kila mwombaji atalipia ada ya FOMU ya Tsh.15,000/=kupitia NMB BANK akaunti
Na. 2101100012 yenye jina UTAWALA CHUO CHA SANAA
- Maombi yaambatanishwe na stakabadhi ya malipo (Receipt/Bank Pay Slip) ya Tsh.
15,000 kwa ajili ya FOMU.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31/05/2015 na maombi yote yatumwe kwa; MTENDAJI MKUU, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania.
- Kwa MAELEZO zaidi wasiliana nasi kupitia namba za simu: 0715974100, 0763408792, na 0715394933 au Barua pepe taasisisanaa@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)