Taarifa kutoka Sikika kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taarifa kutoka Sikika kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015

Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM


kuhusu Sikika na Mswada wa ‪#‎CyberCrimeBill‬.


Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na  Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.


Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh  Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.


Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa  njia ya email kwa Mkiti Kamati Mh Peter Serukamba.


Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau  wanaoda iwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.


Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba ‪#‎CiberCrimeBill‬ iliyopitishwa ina  mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.

Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.

Irenei Kiria
Mkurugenzi wa Sikika
4 Aprili 2015.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages