Shamy tours ya zanzibar yapata leseni ya utalii sweden - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Shamy tours ya zanzibar yapata leseni ya utalii sweden

IMG_2176
Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Bw. Khamis Mwinjuma Simba akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wakati wa zoezi la kugawa zawadi za vinyago kwa wageni waalikwa zaidi ya 300 waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden katika mji wa Trollhattan.Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hii www.shamytours.co.tz

Na Mwandishi Maalumu,Trollhattan, Sweden
KAMPUNI ya kupokea wageni ya Zanzibar ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, imefungua ofisi nchini Sweden ambayo itakuwa inashughulikia masuala ya watalii na wageni mbalimbali wanaotaka kuingia Tanzania na visiwani Zanzibar.

Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy, Khamis Mwinjuma Simba akizungumza mjini hapa alisema kwamba kampuni yake kupitia Bodi ya Utalii ya Sweden wamepata kibali na leseni ya kuanzishwa kwa branchi ya kampuni hiyo yenye makao makuu yake mjini Zanzibar , mtaa wa Malindi.

Kampuni hiyo ambayo tangu kuanzishwa kwake ina miaka minne sasa ilifanya uzinduzi wa branchi yake hivi karibuni, kazi iliyofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dora Msechu wakati akizindua mgahawa wa Mtanzania, Issa Kapande wiki iliyopita.
Simba alisema kwamba tangu kuanzishwa kwake wamepata maendeleo makubwa hasa katika kukabiliana na changamoto za soko na kwamba kwa kuanzishwa kwa tawi hilo wanaangalia kufikia nchi 30 za Ulaya zinazotumia viza ya Ulaya.
IMG_2100
Alisema kuwa na ofisi nchini Sweden kumeamsha mori wa kuongeza mafanikio ya kampuni ili kusaidia juhudi za Wizara ya Utalii Zanzibar katika kuhakikisha kwamba sekta ya Utalii inaendesha uchumi wa Zanzibar.

Alisema wizara kama wizara imefanya juhudi kubwa kuhakikisha utalii unakua na kuleta mafanikio kwa Zanzibar na hivyo ni wajibu wao kama Shamy Tours kuhakikisha kwamba wanatoa fursa walizowezeshwa na wizara hiyo kutanua shughuli zao ili kuihakikishia mapato serikali kwa kuingiza wageni wengi zaidi.

"Tumepata faida kubwa kama Shamy Tours kutoka kamisheni ya utalii hasa usajili, kupewa hati za uendeshaji na vipeperushi na machapisho mbalimbali na hasa chapisho la Karibu Zanzibar linalohusu Zanzibar," alisema Simba na kuongeza kuwa kwa kusaidiwa huko wameweza kusonga mbele na katika miaka minne kwa kushirikiana na Issa Kapande, Mtanzania mbaye amefungua mgahawa wa Kitanzania nchini Sweden, wameweza kuanzisha branchi nchini Sweden.
Alisema pamoja na kuzindua ofisi yao, wameitumia siku ya ufunguzi wa mgahawa wa Issa Kapande kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini Sweden na kuwapatia zawadi halisi za Kitanzania kuwapa ushawishi wa kuja nchini.
IMG_2182
Balozi wa Shamy Tours and Travel Agent nchini Sweden, Bi. Anab akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa wageni waalikwa zilizotolewa na kampuni hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden.
Baadhi ya zawadi hizo ni vinyago vya kimakonde taswira za Wamasai na vipeperushi mbalimbali.
Alisema kuwapo kwa Shammy Tours nchini Sweden kutakuza biashara ya utalii.
Alisema mipango ya kuanzisha ofisi nchini Sweden ilianza zamani wakati Issa Kapande akifanya shughuli zake katika Hoteli ya African House miaka sita iliyopita na kushika kasi katika miaka miwili iliyopita ambapo Issa Kapande alifika Zanzibar mara mbili kukamilisha ushirikiano uliozaa ofisi hiyo ya Sweden.
Alisema pamoja na kujitangaza katika nchi zaidi ya 30 za Ulaya kupitia ofisi hiyo ya Sweden Shamy Tours inatarajia kushiriki katika maonesho ya utalii Afrika Kusini yatakayofanyika Mei mwaka huu, Urusi Juni mwaka huu na London, Uingereza Novemba mwaka huu.
Alisema ushiriki wao ni sehemu ya kutafuta masoko na kuitangaza Tanzania, nchi ya visiwa vya Zanzibar, mlima Kilimanjaro na mbuga ya Serengeti.
IMG_2194
Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hii www.shamytours.co.tz

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages