Pages

Samsung Tanzania yazitambulisha Simu aina ya Samsung S6 Flat na Edge

 Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Tanzania Hyeong Jun Seo akionyesha moja ya simu aina ya Samsung S6 Flat katika uzinduzi wa simu mpya za samsung aina ya Samsung S6 flat na Samsung S6 Edge uliofanyika katika hoteli  ya Hyatt Regence Jijini Dar Es Salaam Jana
 Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Tanzania Hyeong Jun Seo akionyesha moja ya simu aina ya Samsung S6 Edge
 
 Mkuu wa Simu kutoka Samsung Tanzania Sylivester Manyara akielezea sifa za simu hizo samsung S6 Flat na Edge katika uzinduzi wa simu hizo uliofanyika Jijini Dar Jana katika Hotel ya Hyatt Regence huku Sifa moja ya Simu hizo zikiwa na Uwezo wa Kuchaji bila waya ya chaji kuchomekwa kwenye simu (wireless charge) huku kamera ya mbele ikiwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha na Ikiwa na IOS.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regence jijini Dar Jana
Katibu mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia (aliyeshika simu) akiingalia moja ya simu aina ya samsung s6 edge huku akipewa maelezo juu ya uwezo wa simu hizo huku ikiwa imetengenezwa kwa uimara wa hali ya juu kwa kutumia teknolojia ya Gorila inayoipa uwezo kioo cha simu hiyo kuendelea kuwa imara hata ikindondoka.Picha zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)