Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imesaini mkataba na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye gharama ya USD 2,244,376/- milioni (sawa na Tsh 4.1/- bilioni) kwa ajili ya kupeleka mawasiliano ya simu katika kata 19, yenye vijiji 76.
Kata hizo zinatakazonufaika na mradi huu ni pamoja na; Gelai Meirugoi, Arash na Olbalbal- Arusha, Mbondo - Lindi, Makame Shambarai na Masieda- Manyara. Kata nyingine ni pamoja na Ivuna - Mbeya, Masagati na Mombo- Morogoro, Vikumbulu- Pwani, Ligera. kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma zipo kata ya Lukumbule, Marumba, Nakapanya na Nampungu. Aidha kwa mkoa wa Singida zipo kata za Minyughe na Urughu, mwisho kata ya Ubangaa iliyopo mkoa wa Tanga.
Mkataba ambao leo unasainiwa rasmi, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) itatoa huduma za kawaida za mawasiliano ya simu yaani maongezi na huduma za ujumbe mfupi (SMS) na Intaneti.
Mradi huu utakapokamilika, utaleta chachu ya ukuaji wa wa maendeleo katika kata hizo ikiwa ni pamoja na; wananchi wataweza kuwasiliana na pande zote za dunia, kupata na kutumia taarifa za kibiashara, kupata habari za masoko mapya na za kijamii.
Aidha, huduma hii itawawezesha kutoa fursa sawa na watu wa maeneo ya mijini ili kuendelea kujenga uwiano sawa wa kupata na kutoa taarifa kwa maendeleo ya jamii.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)