Je,miraa inaongeza nguvu za kiume? - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Je,miraa inaongeza nguvu za kiume?

Mtu anayekula miraa kenya
Wanaume katika eneo la Meru mashariki mwa Kenya ambao hawana uwezo wa kuwatosheleza wake zao kupitia tendo la ngono sasa wametakiwa kutokuwa na wasiwasi.
Mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo Florence kajuju ameanza mpango wa kuwahamasisha wanaume kutumia miraa badala ya ya pombe haramu .
Akizungumza na gazeti la The Nairobian nchini Kenya,kiongozi huyo amesema kuwa pombe haramu hushusha nguvu za kiume na kuwafanya wanaume kushindwa kuwatosheleza wake zao.
''Ni pombe kama hizi ambazo huathiri nguvu za kiume na kusababisha utasa miongoni mwa wanaume'',alisema.
Kajuju ambaye anasema anapenda miraa aliudhika alipogundua kwamba eneo la Meru ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaume hawana uwezo wa kutafuta watoto.
''Vijana wetu wameathirika vibaya na pombe haramu na lazima tuwaokoe''.
Alisema kuwa wale waliopiga marufuku uuzaji wa miraa katika mataifa yao wanafaa kugundua umuhimu wa zao hilo miongoni mwa jamii.bbc 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages